Mtu ambaye amemwamini Yesu lakini akafa bila kubatizwa je! atenda mbinguni?

0
5K

JIBU: Inategemea kama hapo kabla alishausikia ukweli au la, kwa mfano kama mtu alishaufahamu ukweli tangu zamani, na hataki kufanya hivyo au anapinga, huyo mtu atahukumiwa…Lakini kama huyo mtu ndio mara yake ya kwanza kuamini na kwa bahati mbaya akafa kabla ya kubatizwa, ataokolewa atafananishwa na yule mhalifu pale msalabani aliyekufa na Bwana.

Lakini Wapo watu baada ya kuujua ukweli, hawataki kuufanya uteule wao na wito wao imara kulingana na 2Petro 1: 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

Kadhalika biblia inasema pia katika

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. “

Soma tena hapa..

Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”.

Hivyo masuala ya rohoni ni ya kuyatimiza kwa kuogopa na kutetemeka, na sio ya kuyachukulia tu kijuu juu.. Tunapoujua ukweli na mapenzi ya Mungu tunapaswa kuyafanya.

Wafilipi 2:12”…. utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka”.

Ubarikiwe.

Search
Categories
Read More
DARASA LA 1
DARASA LA 1
Orodha ya masomo yote ya darasa la 1
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:14:04 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Bwana Aliposema Kuwa Yeye Ni “Mungu Wa Miungu” Alikuwa Na Maana Gani?..Je! Yeye Ni Mungu Wa Sanamu?
JIBU: Tukisoma Kumbukumbu 10:17 inasema… “Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:14:03 0 6K
OTHERS
ATHARI YA MKRISTO KUOANA NA MUISLAMU
Imeletwa kwenu na Abel Suleim Shiriwa Imekuwa ni jambo la kawaida kushuhudia Wakristo na...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:04:02 0 9K
Injili Ya Yesu Kristo
KUNYAKULIWA KWA KANISA
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:43:59 0 5K
REVELATION
UFUNUO 12
MAELEZO JUU YA “UFUNUO 12” Ufunuo 12 1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni;...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:35:41 0 5K