JE, UNAWEZA KUOKOKA BILA YA KUPITIA YESU?

0
5Кб
Je naweza kuingia mbinguni bila kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wangu?
Jibu: Hapana, huwezi kwenda mbinguni kama unakataa kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Mambo manne ya kuzingatia kwenye jibu hili.
 
Haki: Mungu ni mwema, Mtakatifu, mwenye haki kwa watu wote (Waebrania 6:10). Mungu huwahukumu watu kwa kuzingatia ufahamu walio nao (Warumi 4:15; 5:13). Abraham hakujua jina la Yesu, lakini alimfuata Mungu na bado aliokolewa kupitia Yesu. (Yohana 8:56, Waebrania 9)
 
Njia moja tu: Hatuwezi kwenda mbinguni kwa kutegemea haki yetu wenyewe; tunahitaji rehema na neema za Mungu kupitia kwa Yesu. Yesu siyo tu njia ya kwendea kwa Mungu bali pia ni njia pekee ya kwendea kwa Mungu. (Yoh 14:6; 15:5; Matendo 4:12). Njia pekee ya kuifikia mbingu ya Mungu ni kupitia njia ya Mungu.
 
Ukimkataa Yesu kama Mwana wa Mungu utakuwa umeikataa mbingu: Hata kwa mtu anayeshika dini sana, Farisayo wa kiyahudi, Yesu alisema kuwa kama ukinikataa utakufa kwenye dhambi zako. (Yohana 8:24)
 
Mungu hutafuta: Mungu hapendi mtu yoyote aangamie (2 Petro 3:9), lakini kama Yeremia alivyowalilia watu wake (Yeremia 13:17; 14:17) na kama Yesu alivyoililia Yerusalem (Luka 19:41-44) na kama Petro alivyowasihi watu waliokuwa wanamsikiliza (Matendo 2:40), Mungu, huwatafuta watu wake kwa haja hiyo hiyo.
 
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom.
Поиск
Категории
Больше
OTHERS
ETI, YESU ALIPOKUWA AMEKUFA DUNIA ILIKUWA INAENDESHWA NA NANI?
Hili ndilo swali la wafuasi wa Muhammad kwa Wakristo na leo nitalijibu hapa.   Hili ni swali...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:42:36 0 6Кб
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:38:19 0 5Кб
OTHERS
MAPEPO (MAJINI) NI NINI HASA?
SEHEMU YA KWANZA Somo:MAPEPO Lengo Kuu: Kujua mapepo na kazi zake. Lengo Mahsusi: Kujua namna ya...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 20:04:19 0 7Кб
REVELATION
MAJIRA YA KANISA LA THIATIRA
(1) MLENGWA WA KANISA{UFUNUO 2:18}Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo...
От GOSPEL PREACHER 2021-09-24 09:47:12 2 7Кб
Injili Ya Yesu Kristo
NI NINI MAANA YA “ROHO”?
Hebu tuzungumzie jinsi Biblia inavyotumia neno “roho.” Watu fulani hufikiri kwamba...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:51:05 0 7Кб