JE, UNAWEZA KUOKOKA BILA YA KUPITIA YESU?
Veröffentlicht 2021-12-24 21:01:24
0
5KB
Je naweza kuingia mbinguni bila kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wangu?
Jibu: Hapana, huwezi kwenda mbinguni kama unakataa kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Mambo manne ya kuzingatia kwenye jibu hili.
Haki: Mungu ni mwema, Mtakatifu, mwenye haki kwa watu wote (Waebrania 6:10). Mungu huwahukumu watu kwa kuzingatia ufahamu walio nao (Warumi 4:15; 5:13). Abraham hakujua jina la Yesu, lakini alimfuata Mungu na bado aliokolewa kupitia Yesu. (Yohana 8:56, Waebrania 9)
Njia moja tu: Hatuwezi kwenda mbinguni kwa kutegemea haki yetu wenyewe; tunahitaji rehema na neema za Mungu kupitia kwa Yesu. Yesu siyo tu njia ya kwendea kwa Mungu bali pia ni njia pekee ya kwendea kwa Mungu. (Yoh 14:6; 15:5; Matendo 4:12). Njia pekee ya kuifikia mbingu ya Mungu ni kupitia njia ya Mungu.
Ukimkataa Yesu kama Mwana wa Mungu utakuwa umeikataa mbingu: Hata kwa mtu anayeshika dini sana, Farisayo wa kiyahudi, Yesu alisema kuwa kama ukinikataa utakufa kwenye dhambi zako. (Yohana 8:24)
Mungu hutafuta: Mungu hapendi mtu yoyote aangamie (2 Petro 3:9), lakini kama Yeremia alivyowalilia watu wake (Yeremia 13:17; 14:17) na kama Yesu alivyoililia Yerusalem (Luka 19:41-44) na kama Petro alivyowasihi watu waliokuwa wanamsikiliza (Matendo 2:40), Mungu, huwatafuta watu wake kwa haja hiyo hiyo.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom.
Suche
Kategorien
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Mehr lesen
JINSI YA KUMJUA MWENZI WAKO ALIYEKUSUDIWA NA MUNGU
Leo napenda tuangalie mambo yatakayokufanya umjue mwenzi wako wa ndoa uliyekusudiwa na Mungu....
Verse by verse explanation of Joshua 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
KAMA YESU NI MUNGU, KWANINI ALIKUFA?
JE, MUNGU ANAKUFA?
Hayo ni maswali ya Waislam kila siku, na kwenye hii mada nitayajibu.
SOMA: 1...
KUBOMOA MADHABAHU ZA SHETANI
Madhabahu ni nini?
Ni daraja la kuunganisha katika ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani.
Kuna...
UKWELI KUHUSU HAKI IPATIKANAYO KWA IMANI
Leo ndugu zangu napenda kuzungumza haswa juu ya kuhesabiwa haki. Je, tunahesabiwaje? Je, kwa...