Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga (ndoa za wanaume kwa wanaume)? Je, Ushoga ni dhambi?

0
5χλμ.
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
 
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
Αναζήτηση
Κατηγορίες
Διαβάζω περισσότερα
Injili Ya Yesu Kristo
SIRI ZA KIROHO ZILIZOPO NDANI YA SIKUU 7 ZA KIYAHUDI
Baada ya wana wa Israeli kutoka Misri na kuingia katika nchi yao ya ahadi Mungu aliwaagiza...
από GOSPEL PREACHER 2023-07-16 00:04:43 2 8χλμ.
SPIRITUAL EDUCATION
MIKATABA INAYOTOKANA NA KAFARA
Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima    Utangulizi: Wakristo wengi huwa hawazungumzii...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:28:30 0 5χλμ.
OTHERS
VLOOKUP function
Use VLOOKUP when you need to find things in a table or a range by row. For example, look up a...
από PROSPER HABONA 2024-01-01 20:56:17 0 3χλμ.
Injili Ya Yesu Kristo
UNAUTUMIAJE UPAKO WA MUNGU JUU YAKO?
Mathayo 21:28-32 – Ukisoma andiko hili utaoona habari  baba mmoja aliyekuwa na...
από GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:23:25 0 5χλμ.
TANZANIA
WELCOME TO PROSHABO ONLINE SCHOOLS
Our online system can be accessed by CLICKING HERE, if you have any problem in clicking this...
από PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-30 07:08:06 0 6χλμ.