Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga (ndoa za wanaume kwa wanaume)? Je, Ushoga ni dhambi?

0
5KB
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
 
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
Pesquisar
Categorias
Leia mais
Injili Ya Yesu Kristo
ZIJUE FUMBO ZA ADUI SHETANI ILI ZISIKUNASE
Kati ya yale makanisa 7 tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Thiatira, lilikuwa ni la...
Por GOSPEL PREACHER 2023-08-19 23:32:40 0 8KB
Injili Ya Yesu Kristo
USIPOKUWA NA WAZO JIPYA HUWEZI KUTOKA MAHALI ULIPO
Salaam katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Katika waraka wa Oktoba 2016 nimeona umuhimu wa...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:32:24 0 6KB
SPIRITUAL EDUCATION
VITA INAYOENDELEA JUU MBINGUNI
Zipo vita mbili kuu zinazowahusu shetani na Malaika watakatifu. Vita ya kwanza: Ni ile...
Por GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:35:03 0 6KB
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 95 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:22:54 0 6KB
SPIRITUAL EDUCATION
Malaika Waliofanya Dhambi
Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Roho na kwamba viumbe wake wa kwanza walikuwa roho. (Yohana...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:35:16 0 5KB