WANAWAKE KUMTUMIKIA MUNGU

0
5KB
Ni uongo wa Shetani kwamba wanawake hawawezi kuwa Watumishi wa Mungu, wakahubiri, wakafundisha, wakatoa pepo au kumtumikia Mungu kwa namna nyinginezo.  Wanawake kumtumikia Mungu, ni jambo la Ki-Biblia hasa. 
 
Nyakati hizi za mwisho, Roho wa Mungu atamwagwa kwa WOTE, binti watatabiri (kuhubiri ni kutabiri pia) na Roho huyu wa Mungu atamwagwa kwa WATUMISHI WA MUNGU WANAUME NA WANAWAKE (MATENDO 2:17-18).  
 
Nyakati za Kanisa la Kwanza, wanaume na wanawake, wote walikuwa watendakazi, wakilihubiri Neno na kulifundisha (MATENDO 8: 1, 4).  Inatupasa kufuata mfumo huu wa ki-Biblia.  Mara kwa mara, katika Biblia, wanawake, wamekuwa na ujasiri wa kumtumikia Mungu na kuwa wanyenyekevu na watii kwa Yesu Kristo na Neno lake, kuliko wanaume.  Hapa tunaona wanawake waliomfuata Yesu kutoka Galilaya, karibu maili 100 kutoka Yerusalemu, wakija kumtumikia Yesu.  Hapa msalabani, hawakuwako wanafunzi wale kumi na moja wa Yesu kasoro Yohana (YOHANA 19: 25-26).  Wengi walikuwa wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea (LUKA 23:27).  
 
Wanawake walikuwepo msalabani mpaka mwisho na tena walikuwapo kwenye mazishi yake (MST 61) na pia wanawake ndiyo waliokuwa wa kwanza kwenda kulitazama kaburi siku ya kufufuka kwa Yesu (MATHAYO 28:1).  Mwanamke ndiye aliyewapelekea habari za kufufuka kwa Yesu, Petro na Yohana, na kuwatia moyo, NDIPO nao wakachangamka!  Hapo mwanzo, walikuwa wamekata tamaa na kwenda kuvua samaki (YOHANA 20:1-3; 21:1-3).  
 
Mwanamke Priska au Prisila alikuwa tayari kukatwa kichwa kwa ajili ya Injili aliyokuwa anaihubiri Paulo na Mwanamke Fibi aliwasaidia wengi mno (WARUMI 16:1-3).  Shime wanawake, tutende kazi ya Bwana! Wanaume pia tupate changamoto kwa watendakazi wanawake ambao wanatenda kazi ya Mungu kwa bidii pamoja na majukumu mengi ya kifamilia waliyo nayo.
Pesquisar
Categorias
Leia mais
OTHERS
Isaac (Christian) or Ishmael (Islam)
Bible = Genesis 17:18,19 “And Abraham said unto God, O that Ishmael might live before thee!...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:23:35 0 5KB
PRE-UNIT
PRE-UNIT 1
List of all of subjects for pre-unit 1 students
Por PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:08:46 0 6KB
REVELATION
UFUNUO 10
Shalom…Karibu katika mwendelezo wa Kitabu cha Ufunuo..ambapo leo kwa Neema za Bwana...
Por GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:05:02 0 5KB
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 53 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:41:10 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
KIUMBE ASIYE KUWA WA ASILI
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Por GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:39:37 0 6KB