KWANINI SULEIMAN ALIKUWA NA WAKE MIA SABA (700) NA MASURIA MIA TATU (300)?
Posted 2021-12-24 21:03:13
0
5K
Kwenye 1 WaFalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumb 17:17?
Jibu: Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Fal 11:1-4 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.
Hard Sayings of the Bible uk.229 inalitumia jambo hili kwa njia ya kupendeza sana. Ingawa Suleiman angeweza kuweka viwango vya juu kama mfano, alianza kujiona kama hana haja ya kuzuiliwa na Mungu kwa njia hii. Leo hii kama kiongozi wa kikristo anajiona kuwa hayumo kwenye mipaka ambayo Mungu ameiweka kwa Wakristo wa kawaida, kiongozi huyu atakuwa kwenye shida kubwa sana ya kiroho. Kwenye Kurani, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuwa na zaidi ya wake wanne, isipokuwa Muhammad tu, ambaye alitokea kuwa na wake karibu 24 baada ya Khadija, na Masuria kumi na wawili.
Zaidi ya hayo, Muhammad na Waislam wengine walikuwa na wasichana mateka na watumwa, na Kurani inawaruhusu Waislam kufanya tendo la ndoa na wanawake ambao wanawamiliki kwa nguvu ya mikono yao. (Sura 4:24; 23:5-6; 70:29-30; 33:50,52 Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150 uk.577)
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom
Căutare
Categorii
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Citeste mai mult
Verse by verse explanation of 1 Kings 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
NAJUTA KWA NINI NILIKUBALI KUOLEWA?
Baada ya mwaka mmoja wa ndoa, Merian asema anajuta kwa nini alikubali kuolewa. Merian na Joseph...
JAMBO LA MSINGI KUZINGATIA KWA WAIMBAJI / VIONGOZI WA SIFA
Ni ujumbe muhimu kwa kila Muimbaji kusoma’
Zaburi 150:1 “Haleluya, Msifuni Mungu...
UTATA: NUHU WA QURAN NI TOFAUTI NA NUHU WA BIBLIA
Ndugu Msomaji:
Siku zote Waislam huwa mnatutambia kuwa, Quran ni kitabu kilichoeleza kila...
Verse by verse explanation of Joshua 24
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...