KWANINI SULEIMAN ALIKUWA NA WAKE MIA SABA (700) NA MASURIA MIA TATU (300)?
Posted 2021-12-24 21:03:13
0
5K
Kwenye 1 WaFalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumb 17:17?
Jibu: Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Fal 11:1-4 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.
Hard Sayings of the Bible uk.229 inalitumia jambo hili kwa njia ya kupendeza sana. Ingawa Suleiman angeweza kuweka viwango vya juu kama mfano, alianza kujiona kama hana haja ya kuzuiliwa na Mungu kwa njia hii. Leo hii kama kiongozi wa kikristo anajiona kuwa hayumo kwenye mipaka ambayo Mungu ameiweka kwa Wakristo wa kawaida, kiongozi huyu atakuwa kwenye shida kubwa sana ya kiroho. Kwenye Kurani, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuwa na zaidi ya wake wanne, isipokuwa Muhammad tu, ambaye alitokea kuwa na wake karibu 24 baada ya Khadija, na Masuria kumi na wawili.
Zaidi ya hayo, Muhammad na Waislam wengine walikuwa na wasichana mateka na watumwa, na Kurani inawaruhusu Waislam kufanya tendo la ndoa na wanawake ambao wanawamiliki kwa nguvu ya mikono yao. (Sura 4:24; 23:5-6; 70:29-30; 33:50,52 Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150 uk.577)
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom
Zoeken
Categorieën
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Read More
Kujengwa kwa Hekalu bila kelele!
1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa...
Verse by verse explanation of Judges 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
Where Do We Go When We Die?
Because he is the only one who died and came back to life on the third day, Jesus knows more...
STANDARD 4
List of all subjects for the standard 4 class
Book of Ruth Explained
Title: Ancient versions and modern translations consistently entitle this book after Ruth...