Kujichua/punyeto – je, ni dhambi kulingana na Biblia?

0
6Кб
Biblia haitaji kujichua wala kwamba kujichua ni dhambi. Hakuna swali juu ya kuwa kitendo kinachoelekeza mtu katika kujichua ni dhambi pia. Kujichua ni kitendo cha mwisho katika kuwasilisha ujumbe wa tamaa mbaya, inayotokana na msisimko wa hisia za ngono ama kutazama kanda za video za ngono. Haya ndiyo matatizo ambayo ni tuyatatue. Ikiwa dhambi ya tamaa na kuangalia picha za ngono itaachwa na kushindwa –shida ya kujichua itaisha.
 
Biblia inatuagiza kuepuka hata hali ya kutazama matendo machafu ya ngono (waefeso 5:3). Sioni kuwa kujichua kutashinda mtihani huu. Mara nyingi kitu ambacho unaaibika nacho huwa ni dhambi. Na hata hivyo kwa kuwa hatuwezi kumuomba Mungu akibariki kitendo cha kujichua ili akitumie kwa wema wa jina lake inaonyesha wazi kwamba ni dhambi. Hatuwezi kujisikia tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanya kitendo hicho cha kujichua.
 
Biblia inatufundisha, “kwa hivyo mkila au mkinywa chochote mkifanyacho, kifanyeni kwa utukufu wa Mungu” (wakorintho wa kwanza 10:31). Kama hakuna uhakika wa kumpendeza Mungu basi heri kukiacha kitendo hicho. Kitendo cha kujichua ni cha kuonewa shaka. “kwa kuwa chochote ambacho si cha imani ni dhambi” (warumi 14:23). Lazima tujue ya kwamba miili yetu pamoja na roho zetu zimekombolewa na ni za Mungu. “Nini? Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu kwa ajili ya Mungu na ninyi si mali yenu wenyewe? Kwa kuwa mmenunuliwa kwa thamani; kwa hivyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu na katika roho zenu ambavyo vyote ni vya Mungu” (wakorintho wa kwanza 6:19 -20). Ukweli huu lazima uwe na mizizi ndani ya maisha yetu kokote tuendako na chochote tufanyacho. Kwa sababu ya haya yote ninasema kujichua ni dhambi kwa mujibu wa Biblia. Siamini kujichua kunaweza kumpendeza Mungu, kwa kuwa kunaepuka mipaka ya heshima na sheria ya Mungu juu ya miili yetu.
Поиск
Категории
Больше
Injili Ya Yesu Kristo
Msikilizeni Israel, Baba yenu!
Mstari wa Msingi:- Mwanzo 49:1-2 “Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili...
От GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:36:48 0 7Кб
STANDARD 7
STANDARD 7
List of all subjects for the standard 7 class
От PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:21:57 0 6Кб
FORM 2
FORM 2
List of all subjects for the form 2 class AGRICULTURE BASIC MATHEMETICS BIOLOGY BOOK-KEEPING...
От PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:23:39 0 6Кб
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 26
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 55 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-24 15:16:54 0 6Кб
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 23
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 22 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-25 08:42:07 0 6Кб