Ni kwa nini uzao wa ubikira ni wa maana?

0
5K
 Funzo la uzao wa ubikira ni la maana sana (Isaya 7:14 Mathayo 1:23; Luka 1:27,34). Kwanza, hebu tuangazie vile bibilia inavyo lieleza swala la uzao wa ubikira. Kulingana na swali la Mariamu, “Litakuwaje neno hili?” (Luka 1:34), Gabrieli anasema, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu” (Luka 1:35). Malaika alimtia moyo Zekaria isiwe na hofu mchukue Mariamu kama mke wako kwa maneno haya: “mimba aliyoibeba ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu” (Mathayo 1:18). Wagalatia 4:4 pia yafunza juu ya uzao wa ubikira “Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke.”
 
Kutoka kwa ukurasa huu, ni kweli kwamba kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa kwa Roho Mtakatifu uliofanya kazi ndani ya Mariamu. Roho usio na mwili na mwili (tumbo ya Mariamu) vyote viliusika. Mariamu hangeweza kujitia mimba, kwa hali hiyo alitumika kama “chombo” ni Mungu pekee angeweza kutenda muujiza wa mwili na kuchukua ule wa mwanadamu.
 
Kukataa upatanisho wa Mariamu na Yesu itamaanisha kwamba Yesu hakuwa binadamu kabisa. Maandiko yafunza kwamba Yesu alikuwa binadamu, mwili kama wetu. Huu aliupokea kutoka kwa Mariamu. Kwa wakati huo, kikamilifu Yesu alikua Mungu, akiwa na mwili wa milele usio na mawaa (Yohana 1:14; 1Timotheo 3:16; Waebrania 2:14-17.)
 
Yesu hakuzaliwa kwa dhambi; hiyo ni kusema hakuwa na hali ya dhambi (Waebrania 7:26). Itaonekana kuwa hali ya dhambi itapitishwa kutoka kizazi hadi kizazi kingine kupitia kwa baba (Warumi 5:12, 17, 19). Uzao wa ubikira wa Yesu haukufuata hali ile ya kupitisha dhambi kutoka kizazi hadi kizazi na kumruhusu Mungu aishiye milele kuwa mwanadamu kamili.
Search
Categories
Read More
OTHERS
EVOLUTION IS SATANISM!! Abortion Holocaust
If I were you I would BLOW UP MYSELF!Your existence is totally POINTLESS.This was my way of...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:32:07 0 5K
PSALMS
Verse by verse explanation of Psalm 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 19 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-05-20 11:57:31 0 8K
OTHERS
UTATA KATIKA KORAN: ADAM ALIUMBWAJE?
Binadamu aliumbwa kutoka nini? Tone la Damu? Maji? Udongo? Vumbi?Jamani huu nao ni Msiba Mkubwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:20:59 0 5K
FORM 1
BASIC MATHEMATICS: FORM 1
List of all topics in Basic Mathematics for form 1 class: CLICK HERE TO VIEW. NUMBERS FRACTIONS...
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 12:44:29 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
MUNGU HANA DINI
Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:31:19 0 6K