Ukijibu Kabla Haujasikia, Ni Upumbavu Na Aibu Kwako.

0
6K

Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,  Ni upumbavu na aibu kwake.


Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?

Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake. 

Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii. 

Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.

Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.

Yohana 8:52-53

[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo  yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)

Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.

Yakobo 1:19

[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Bwana akubariki.

Like
1
Search
Categories
Read More
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 5
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-19 19:29:47 0 5K
UCHUMBA KIBIBLIA
MAMBO YA KUFANYA/KUZINGATIA KATIKA KIPINDI CHA UCHUMBA
Mpenzi msomaji tunakusalimu kwa jina la Yesu! Baada ya kuwa tumepata maombi ya vijana wengi...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:25:47 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
YESU NDIE NJIA NA KWELI NA UZIMA. Kumbe Dini sio Njia
Katika Biblia tunasoma kuwa Yesu anasema yeye ndie "KWELI" na anaendelea kusema kuwa KWELI ndiyo...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:34:15 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Ubatizo Wa Roho Mtakatifu
Mtu anaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, utendaji wa Roho Mtakatifu katika kanisa la kwanza...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:37:38 0 5K
OTHERS
UTATA KATIKA UUMBAJI WA MAJINI
ALLAH: UTATA KATIKA UUMBAJI WA MAJINIJe, Majini yaliumbwaje?Leo hii tutajifunza UTATA wa Allah...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:20:08 0 4K