Ukijibu Kabla Haujasikia, Ni Upumbavu Na Aibu Kwako.

0
6K

Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,  Ni upumbavu na aibu kwake.


Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?

Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake. 

Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii. 

Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.

Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.

Yohana 8:52-53

[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo  yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)

Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.

Yakobo 1:19

[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Bwana akubariki.

Like
1
Tafuta
Vitengo
Soma Zaidi
REVELATION
UFUNUO 15
Karibu tujifunze mwendelezo wa kitabu cha ufunuo, leo tukiendelea na sura ya 15; Ufunuo...
Kwa GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:50:48 0 6K
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
5 Money Mistakes That Lead to Debt
Here are five common money mistakes that can quickly lead to debt. Avoid them at all costs. 1....
Kwa BIBLICAL FINANCES 2021-12-29 15:51:36 0 9K
Injili Ya Yesu Kristo
HAZINA ILIYOSITIRIKA NA MFANYABIASHARA
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Mkuu Zachary Kakobe      ...
Kwa GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:43:14 0 5K
OTHERS
KUMBE KORAN HAIKUTEREMSHWA KUTOKA KWA ALLAH
Ni Nani Walikuwa Waandishi Wa Quran Tukufu Wakati Wa Mtume Muhammad? Je, ungependa kuwafahamu...
Kwa MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 18:29:28 0 5K
Networking
How to turn your marketplace into a community
As we have learned in the earlier chapters of the Practical guide for building a...
Kwa Business Academy 2022-09-17 03:49:25 0 9K