HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA SHIDA

0
5K

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki..

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute" Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha" Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya "Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'. Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. BINTI ALIYEMKUFURU MUNGU.

Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti (buti) la gari". Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika. Bila shaka Mungu aliyalinda mayai yale tu, kwa kuwa kule ndiko ambako watoto walipotaka Mungu akae.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia" Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simuhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu

Zoeken
Categorieën
Read More
MASWALI & MAJIBU
Inaruhusiwa Kula Nyama Ya Nguruwe Kwa Mkristo Wa Kweli? Pia Je, Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara?
JIBU LA 1: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:59:21 0 7K
MAHUSIANO KIBIBLIA
SEHEMU YA 5: MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA
Bwana asifiwe!! Unaweza kusoma SEHEMU YA 1, SEHEMU YA 2, SEHEMU YA 3, SEHEMU YA 4 ya somo hili,...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 11:49:18 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28
UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU. 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28. Moja kati ya teso kubwa la...
By Martin Laizer 2025-11-05 04:53:38 1 558
PSALMS
Verse by verse explanation of Psalm 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 38 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-04 22:58:57 0 5K
2 SAMUEL
Book of 2 Samuel Explained
Introduction: See 1 Samuel for the introductory discussion. First and Second Samuel were...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-27 20:29:09 0 6K