Ukijibu Kabla Haujasikia, Ni Upumbavu Na Aibu Kwako.

0
6K

Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,  Ni upumbavu na aibu kwake.


Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?

Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake. 

Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii. 

Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.

Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.

Yohana 8:52-53

[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo  yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)

Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.

Yakobo 1:19

[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Bwana akubariki.

Like
1
Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 25
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 60 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 18:11:03 0 5K
OTHERS
MUHAMMAD ALIKUWA NA DHAMBI KUBWA KIASI CHA KUOMBA MSAMAHA MARA MIA KWA SIKU
Dhambi kubwa Katika "Sahih Muslim, Kitabu 35, 6522 Idadi" inasema kwamba Muhammad alikuwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:14:15 0 5K
OTHERS
KUTEKWA NYARA!! USHUHUDA WA KUSISIMUA
“Nilikamatwa na kuteswa na polisi wa Misri kwa kuhoji imani yangu katika...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:35:20 0 5K
UCHUMBA KIBIBLIA
ATHARI ZA MAHUSIANO YA UCHUMBA YA MUDA MREFU KUPITA KIASI (Miaka 2 au zaidi)
1. Huweza Kufungua Milango ya uasherati kwa WachumbaInaweza kupelekea kwenye maisha ya uasherati...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-08 00:31:44 0 6K
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 24
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 58 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:34:42 0 6K