Ukijibu Kabla Haujasikia, Ni Upumbavu Na Aibu Kwako.

0
6كيلو بايت

Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,  Ni upumbavu na aibu kwake.


Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?

Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake. 

Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii. 

Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.

Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.

Yohana 8:52-53

[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo  yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)

Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.

Yakobo 1:19

[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Bwana akubariki.

Like
1
البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
Religion
MASWALI NA MAJIBU KUHUSU DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU
Kumekuwepo na mijadala mingi kila mahali na pia kumewepo na maoni mengi ya watu na mawao tofauti...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-08-24 13:00:08 0 7كيلو بايت
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-04-02 01:23:16 0 5كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
IJUE BIBLIA YA SHETANI
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote ambao mmeumbwa na mwenyezi MUNGU na siyo shetani...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-11-19 06:47:41 0 5كيلو بايت
Religion
KUMTUMAINI MUNGU
HEKIMA NI KUMTUMAINI MUNGU TU: Huu ndio ukweli hata Kama wapo watakaopinga, lakini ukweli...
بواسطة tabitha Prosper 2021-08-31 06:48:51 0 6كيلو بايت
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:34:26 0 5كيلو بايت