Kuna Ufufuo Wa Aina Ngapi?

0
5K

JIBU: Biblia inasema kuna ufufuo wa aina mbili,

Ufufuo wa kwanza, umejumuisha wale watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu ukisoma (Mathayo 27:52) utaona..,pamoja na watakatifu watakao fufuka katika unyakuo, na watakao fufuliwa wakati wa kuingia kwenye ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 20:4) haya ni makundi matatu yanayotengeneza aina ya kwanza ya ufufuo.  

Ufunuo 20:6 “….Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza, juu ya hao mauti ya pili haina nguvu…”  

Na ufufuo wa pili utakuja mara tu baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha..ambapo wafu wote ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza watafufuliwa na kuhukumiwa na Kristo mwenyewe katika hukumu ya kile kiti cheupe cha Enzi cha Yesu Kristo tukisoma  

Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”

Kwahiyo ndugu biblia inasema wana heri wale watakaokuwepo katika ule ufufuo wa kwanza. kwasababu mauti ya pili haitakuwa na nguvu juu yao. Na mauti ya pili ni ziwa la moto. Hivyo tujitahidi hata kama Bwana atakupokuja akatukuta tumelala(tumekufa), basi tuwe na nafasi katika ule ufufuo wa kwanza.

Ubarikiwe sana.

Zoeken
Categorieën
Read More
REVELATION
MAJIRA YA KANISA LA LAODIKIA
(1) MLENGWA WA KANISAMlengwa hapa ni kanisa lililoko LaodikiaLaodikia ulikuwa ni mji ambao...
By GOSPEL PREACHER 2021-09-24 11:28:48 0 7K
NDOA KIBIBLIA
KIPI KINAHITAJI MAANDALIZI SANA KATI YA NDOA NA HARUSI?
Shalom mpendwa wangu katika Kristo Yesu, Leo katika kona yetu hii ya mahusiano ya uchumba na...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 15:04:24 0 5K
OTHERS
MTUME PAULO ANAVYO WANYIMA USINGIZI WAISLAM
Kati ya watu wanaowasumbua sana ndugu zetu Waislamu ni shujaa wa Bwana Yesu, Mtume Paulo. Na hii...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:04:40 0 7K
DARASA LA 2
DARASA LA 2
Orodha ya masomo yote ya darasa la 1
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:14:30 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
MAANA YA KANISA
Kwanza kabisa neno Kanisa linamaanisha "mkusanyiko wa waamini" kama ule wa Waisraeli chini ya...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 21:00:38 0 6K