Je! kuna dhambi kubwa na ndogo?

0
5K

SWALI: Naomba kufahamu Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?


JIBU: Dhambi ni dhambi iwe kubwa au ndogo, zote ni kosa, biblia inasema.

Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. “

Unaona hapo? Kwahiyo mtu akitenda dhambi iwe kubwa au ndogo ataadhibiwa. lakini adhabu zitatofautiana huko waendako kulingana na wingi wa makosa, kwasababu Bwana Yesu pia alisema aliyeua kwa upanga atauawa kwa upanga, apandacho mtu ndicho atakachovuna. adhabu ya shetani haiwezi ikawa sawa na adhabu ya mwanadamu. Biblia inaeleza..

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, ATAPIGWA SANA. 48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, ATAPIGWA KIDOGO. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi. “

Kwahiyo mapigo yanatofautiana kulingana na matendo ya mtu aliyoyatenda akiwa hapa duniani, ni kama tu vile thawabu zitavyotofautiana kwa mtu na mtu mbinguni kwa jinsi alivyotaabika katika kumtumikia Bwana vivyo hivyo na jehanamu adhabu zitatofautiana kulingana na dhambi mtu alizotenda akiwa ulimwenguni. Na jinsi gani alivyoipuuzia neema ya wokovu.

Hivyo hatupaswi kuipima dhambi kwa namna yoyote, ni kukaa nayo mbali kwasababu iwe ni kubwa au ndogo mshahara wake ni MAUTI, Warumi 6:23.

Dhambi kubwa na ndoto zote zina adhabu ya mauti.

Je! Umempa Yesu maisha yako ndugu yangu? Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho?. Ukifa leo utakuwa mgeni wa nani, huko uendako?. Tubu sasa mgeukie yeye atakusamehe, na kukupa uzima wa milele.

Mungu akubariki.

Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
Je, Yesu anawezaje kuwa Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja?
Ni nini maana ya muungano wa kimwili na Uungu?Hili ni swali linalo ulizwa mara nyingi sana, ni...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 21:14:28 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
KWA NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUMZIMISHA ROHO MTAKATIFU?
Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:55:47 2 6K
MASWALI & MAJIBU
Mitume Wote Waliopita Walikuwa Ni Watu Weupe Hata Manabii Wote Waliopita Hadi Ma-Papa Ni Ngozi Nyeupe. Ni Kweli Ngozi Nyeusi Ililaaniwa ?
JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:37:18 0 5K
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:35:09 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO
Yoshua 13:1-7 Utangulizi, Katika dunia ya leo  watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:42:34 0 5K