YESU ATAKUPONYA.

0
5K

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

“Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.” Luka 5:19-20

Najaribu kukutia moyo kuhusu ugonjwa wa mwili unaopitia sasa,kwamba usikate tamaa kwa maana yupo Mungu aponyaye. Maandiko yanatueleza ile kweli halisi kuhusu uponyaji uliopo ndani ya Yesu. Bila shaka mgonjwa huyu alichukuliwa na watu wanne yeye akiwa hoi kitandani. Ashukuriwe Mungu hawa ndugu wanne walikuwa wapi kwa kumpeleka mgonjwa wao ili apone. Namna tu ya kujua sehemu sahihi ya uponyaji wako nalo ni neno kubwa sana.

Kwa sababu wapo wagonjwa wengi ambao wamekata kauli lakini wale wanaossimamia hawajui mahali sahihi pa kumpeleka,na ndio maana wapo wagonjwa waliopelekwa kwa waganga wa tungulisi kama walikuwa wanapenda au kutaka lakini walijikuta wako kwa waganga wa tunguli,kwa sababu waliomchukua hana maarifa sahihi. Bila shaka mgonjwa hakuwa na maazi ya wapi apelekwe na wapi asipelekwe,labda alikata kauli au labda hana sauti. Lakini tunawapongeza wale waliomchukua na kumpeleka kwa mponyaji,Yesu Kristo wa Nazareti. Yesu huyo huyo yupo hata sasa,ukiamini tu,utapona.

Huyu mgonjwa labda alikuwa wala aamini habari za Yesu,nalo ni jambo la kushangaza. Lakini Yesu alimponya pale alipoiona imani yao wale waliomchukua hata kupangua matofali ya dari / paa la watu. Hawa ndugu walikuwa na akili maana hawakuvunja paa la watu,bali walipangua kwa utaratibu ili wasipate gharama ya kulipa paa. Lakini Yesu alipowaona,aliona imani yao,hii ina maana “imani ” ni muhimu sana ikiwa kama unahitaji kuapona. Ni lazima uamini kwanza,tena na ni vyema ili upokee uponyaji kikamilifu. hata leo ukiomba kwa imani,tegemea kupona hata kama sio leo basi kesho utapona tu. Usife moyo,usikate tamaa yupo Mungu aponyaye hata sasa.

Buscar
Categorías
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
MACHO YA TAI AWINDAE MAWINDO YAKE
Macho ya Tai AWINDAE mawindo yake  Kila mmoja wetu tunapaswa kuwa na macho ya kuona...
By Martin Laizer 2023-09-22 09:29:34 2 18K
Networking
How to find great online marketplace ideas
Perhaps you already have a business idea that you can't get out of your mind. Or maybe you're...
By Business Academy 2022-09-17 03:34:39 0 7K
SPIRITUAL EDUCATION
TENGENEZA MAMBO YA NYUMB YAKO
TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO
By Martin Laizer 2023-12-19 18:47:21 0 6K
JONAH
YONA 4
Bwana wetu YESU KRISTO atukuzwe. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa neema hii mpya ya kujifunza...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-20 03:14:39 0 5K
Networking
Your marketplace MVP – How to build a Minimum Viable Platform
Once you have gone through the initial process of customer discovery, you should have a...
By Business Academy 2022-09-17 03:47:15 0 8K