ALIVYOOKOKA SHEIKH ALHAJI RASHID ABUBAKAR WA MSIKITI WA MTAA WA MWANZA ILALA DAR ES SALAAM
Posted 2021-12-24 21:24:13
0
8K
1. AKIRI KULA NYAMA ZA WATU
2. AKIRI KUNYWA DAMU ZA WATU
3. AKIRI KUMEZA MAJINI 360
4. ASEMA UISLAM NI DINI YA WACHAWI
Ndugu msomaji,
Soma huu ushuhuda wa kusisimua kutoka kwa Sheikh Alhaji Rashid Tahtashajara Abubakar aliye kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360.
Mwenyekiti wa waislamu waliookoka, Afrika Mashariki na Kati!
Alitokea kwenye familia ya kichawi, mama yake alijiita ni Mungu na kufanya miujiza mbalimbali ikiwemo ya kunyesha mvua. Sheikh Alhaji Rashid Tatashajara Abubakar, aliwahi kufanya shughuli za kisheikh katika msikiti wa Ilala mtaa wa Mwanza ambapo pia alikua mwanafunzi wa sheikh Yahaya Hussein ambaye ni marehemu kwa sasa.
Alianza kujifunza madrasa, akapanda vyeo na kusomea vyuo vya kichawi baada ya kuhitimu majaribio mbalimbali ikiwemo kufukua makaburi, kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mkuu wa wachawi Afrika mashariki na kati!
Anasema katika mambo hayo yote, alikua akitumwa kushambulia watumishi wa Mungu mbalimbali, aliwahi kujaribu kwa Moses Kulola, Emmanuel Lazaro na Askofu Mwanisongole. Lakini alishindwa na kupata mieleka iliyompelekea kuumwa sana.
“Siku Moja mtaa wa Salender Bridge kama mliwahi kusikia kisa cha dada aliyeota manyoya, alifikishwa kwangu nikamuombea kwa Jina la Yesu naye akapokea uponyaji. Kwa sasa yuko Marekani! nimemuona Mungu kwa jinsi ya tofauti kule nilikotoka nilikua namtumikia shetani, kwa sasa namtumikia Bwana Yesu, na kila ulimi utakiri kwamba Yesu ndiye Mungu”
Alhaji Rashid Abubakary kwa sasa ni mwenyekiti wa waislamu waliookoka Afrika mashariki na kati. Mungu amekua akimtumia kwa jinsi ya tofauti na amealikwa makanisa mbalimbali na kueleza shuhuda nyingi ambazo Bwana Yesu amefanya na kufanya kwenye maisha ya watu wengine. Ameonekana kwenye Televisheni ya kikristo ATN, ushuhuda huu kwa ufupi ameutoa tarehe 26 Agosti 2011, Kanisa la City Christian Centre.
Search
Categories
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Read More
NAMNA SHETANI ANAVYOTUMIA ROHO YA USAHULIFU KUHARIBU MAISHA YA WAAMINI
Shalom, katika waraka huu wa Desemba 2016 nimeona ni vema kukumbusha juu ya jambo hili...
Book of Genesis Explained
Genesis is the book of beginnings. It records the beginning of time, life, sin, salvation, the...
ISHARA ZA ZAMANI HIZI
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe
Tovuti : http://www.bishopzacharykakobe.org...
Verse by verse explanation of Genesis 47
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
HATUA TATU MUHIMU KABLA YA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mojawapo ya swali gumu kuhusiana na mahusiano ni pale vijana wanapouliza wakae kwenye uchumba kwa...