YESU NDIE NJIA NA KWELI NA UZIMA. Kumbe Dini sio Njia

0
6K
Katika Biblia tunasoma kuwa Yesu anasema yeye ndie "KWELI" na anaendelea kusema kuwa KWELI ndiyo itakuweka HURU. Hebu rejea kwenye hii aya: 

Yohana 14:6 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

Kufuatana na aya hapo juu, Mtu yeyote yule hawezi kwenda kwa Baba na/au Mbiguni bila ya kupitia "KWELI" ambayo ni YESU. Kumbe basi dini haiwezi kukupeleka popote pale. Kumbe, NJIA PEKEE ya Uzima wa Milele ni YESU na SI DINI.

Kumfahamu Yesu ambaye ni KWELI kutakufanya umwelewe Mungu wa UKWELI!! Kumbe basi, Yesu ndie mwenye uwezo wa kukufanya uelewe KWELI ya Mungu.

Yohana 8:31-32 Kwa hiyo Yesu akawaambia wale waliomwamini, “Kama mkiendelea kutii maneno yangu mtakuwa wanafunzi wangu halisi. 32 Mtaelewa yaliyo kweli kumhusu Mungu na ukweli huu utawafanya muwe watu huru.

Kufuatana na aya hapo juu, inatuhakikishia kuwa mafundisho ya YESU PEKEE ndiyo yatakufanya uelewe KWELI na kumfahamu Mungu wa KWELI. Zaidi ya hapo, kuwa Mwanafunzi wa Yesu(Ukristo) ndio njia pekee ya kufahamu kweli.

Yesu Ndie Njia ya Kweli na Uzima.
Buscar
Categorías
Read More
FORM 4
FORM 4
List of all subjects for the form 4 class AGRICULTURE BASIC MATHEMETICS BIOLOGY BOOK-KEEPING...
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:25:06 0 6K
REVELATION
UFUNUO 7
Dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika wakati wa kumalizia, kurudi kwa YESU KRISTO mara...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 10:21:20 0 6K
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 34 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:59:24 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
TAMBUA NAFASI YAKO ULIOITIWA
Nafasi mbili za mkristo katika wokovu
By Martin Laizer 2023-09-28 05:37:50 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
MBWEHA WADOGO WAIHARIBUO MIZABIBU
Wimbo uliobora 2:15 “Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-31 14:34:48 0 8K