JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA
Сообщение 2021-11-19 07:12:46
0
5Кб
- Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA KUMSINGIZIA..."AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA, BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA, ATAPATA REHEMA"(Mithali 28:13).
- Ungama Dhambi Hiyo Kwa Lengo La Kutengeneza Na Mungu..."DHAMBI ZENU ZIMEWAFARAKANISHA NA MUNGU"(Isaya 59:2). Halafu Omba "NGUVU YA MUNGU" Kukusaidia "USIRUDIE KUTENDA DHAMBI ILEILE"... Yesu Alisema, "MAANA PASIPO MIMI, NINYI HAMUWEZI NENO/ JAMBO LOLOTE" (Yohana 15:5). Kuishinda Dhambi, Si Kwa Akili Na Jitihada Ya Kimwili, "SI KWA NGUVU WALA SI KWA UWEZO BALI NI KWA ROHO WA BWANA" (Zekaria 4:6).
- Amua Kwa Dhati KUACHANA NA WATU "WANAOKUSHAWISHI" Au WANAOKUPELEKEA DHAMBINI"... "HERI MTU YULE ASIYEKWENDA KATIKA SHAURI LA WASIO HAKI [Watu Wasioipenda Haki Ya Mungu Na Neno Lake]... WALA HAKUSIMAMA KATIKA NJIA YA WAKOSAJI [Watu Ambao Wao Kutenda Makosa Ni Life Style Yao Na Hawajali Lolote]... WALA HAKUKETI BARAZANI PA WENYE MIZAHA [Makusanyiko Ya Watu Au Vijiwe Ambako Mambo Yasiyomtukuza Mungu Yanapewa Nafasi]"(Zaburi 1:1-2).
- Badili Mfumo Wako Wa Maisha, Toka Katika Ile Njia Ikupelekayo Dhambini Upesi... Amua Kuishi Kwa Ajili Ya Kumpendeza Mungu Kuliko Yeyote Au Chochote... HII INAHITAJI KUBADILI MFUMO WAKO WA MAWAZO [CHANGE OF MIND]... "MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII, BALI MFANYWE UPYA KWA KUGEUZWA NIA ZENU, MPATE KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU YALIYO MEMA, YA KUPENDEZA NA MAKAMILIFU" (Warumi 12:2).
- Dumu Kwenye Maombi Na Ushirika Na Mungu... MAOMBI YATAKUINGIZA KWENYE UWEPO WA MUNGU, NENO LAKE LITAKUFANYA USHIRIKIANE NAYE..."TENA IPOKEENI CHAPEO YA WOKOVU, NA UPANGA WA ROHO AMBAO NI NENO LA MUNGU. KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE"(Waefeso 6:17-18).
Rumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”
Поиск
Категории
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Больше
Verse by verse explanation of 1 Kings 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
ALLAH IS A CREATION AND NOT THE CREATOR
Who is Allah?
the Islamic diabolical deity is called “The Greatest Deceiver”...
Verse by verse explanation of Psalm 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 19 questions at the...
MOTO WA KIGENI
Walawi 10:1-2 “Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake,...
YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO
(basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani wakiyasikiliza...