JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA

0
5K
  1. Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA KUMSINGIZIA..."AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA, BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA, ATAPATA REHEMA"(Mithali 28:13).
  2. Ungama Dhambi Hiyo Kwa Lengo La Kutengeneza Na Mungu..."DHAMBI ZENU ZIMEWAFARAKANISHA NA MUNGU"(Isaya 59:2). Halafu Omba "NGUVU YA MUNGU" Kukusaidia "USIRUDIE KUTENDA DHAMBI ILEILE"... Yesu Alisema, "MAANA PASIPO MIMI, NINYI HAMUWEZI NENO/ JAMBO LOLOTE" (Yohana 15:5). Kuishinda Dhambi, Si Kwa Akili Na Jitihada Ya Kimwili, "SI KWA NGUVU WALA SI KWA UWEZO BALI NI KWA ROHO WA BWANA" (Zekaria 4:6).
  3. Amua Kwa Dhati KUACHANA NA WATU "WANAOKUSHAWISHI" Au WANAOKUPELEKEA DHAMBINI"... "HERI MTU YULE ASIYEKWENDA KATIKA SHAURI LA WASIO HAKI [Watu Wasioipenda Haki Ya Mungu Na Neno Lake]... WALA HAKUSIMAMA KATIKA NJIA YA WAKOSAJI [Watu Ambao Wao Kutenda Makosa Ni Life Style Yao Na Hawajali Lolote]... WALA HAKUKETI BARAZANI PA WENYE MIZAHA [Makusanyiko Ya Watu Au Vijiwe Ambako Mambo Yasiyomtukuza Mungu Yanapewa Nafasi]"(Zaburi 1:1-2).
  4. Badili Mfumo Wako Wa Maisha, Toka Katika Ile Njia Ikupelekayo Dhambini Upesi... Amua Kuishi Kwa Ajili Ya Kumpendeza Mungu Kuliko Yeyote Au Chochote... HII INAHITAJI KUBADILI MFUMO WAKO WA MAWAZO [CHANGE OF MIND]... "MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII, BALI MFANYWE UPYA KWA KUGEUZWA NIA ZENU, MPATE KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU YALIYO MEMA, YA KUPENDEZA NA MAKAMILIFU" (Warumi 12:2).
  5. Dumu Kwenye Maombi Na Ushirika Na Mungu... MAOMBI YATAKUINGIZA KWENYE UWEPO WA MUNGU, NENO LAKE LITAKUFANYA USHIRIKIANE NAYE..."TENA IPOKEENI CHAPEO YA WOKOVU, NA UPANGA WA ROHO AMBAO NI NENO LA MUNGU. KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE"(Waefeso 6:17-18).

Rumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”

Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
ISHARA ZA ZAMANI HIZI
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe Tovuti : http://www.bishopzacharykakobe.org...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:55:23 4 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Msiba katika bonde la kukata maneno!
Yoeli 3:12-14 “Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:31:44 0 5K
JUDGES
Verse by verse explanation of Judges 12
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:01:07 0 5K
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-19 19:23:59 0 5K
JOB
Verse by verse explanation of Job 34
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 23 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:14:29 0 5K