JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA
Postado 2021-11-19 07:12:46
0
5K
- Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA KUMSINGIZIA..."AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA, BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA, ATAPATA REHEMA"(Mithali 28:13).
- Ungama Dhambi Hiyo Kwa Lengo La Kutengeneza Na Mungu..."DHAMBI ZENU ZIMEWAFARAKANISHA NA MUNGU"(Isaya 59:2). Halafu Omba "NGUVU YA MUNGU" Kukusaidia "USIRUDIE KUTENDA DHAMBI ILEILE"... Yesu Alisema, "MAANA PASIPO MIMI, NINYI HAMUWEZI NENO/ JAMBO LOLOTE" (Yohana 15:5). Kuishinda Dhambi, Si Kwa Akili Na Jitihada Ya Kimwili, "SI KWA NGUVU WALA SI KWA UWEZO BALI NI KWA ROHO WA BWANA" (Zekaria 4:6).
- Amua Kwa Dhati KUACHANA NA WATU "WANAOKUSHAWISHI" Au WANAOKUPELEKEA DHAMBINI"... "HERI MTU YULE ASIYEKWENDA KATIKA SHAURI LA WASIO HAKI [Watu Wasioipenda Haki Ya Mungu Na Neno Lake]... WALA HAKUSIMAMA KATIKA NJIA YA WAKOSAJI [Watu Ambao Wao Kutenda Makosa Ni Life Style Yao Na Hawajali Lolote]... WALA HAKUKETI BARAZANI PA WENYE MIZAHA [Makusanyiko Ya Watu Au Vijiwe Ambako Mambo Yasiyomtukuza Mungu Yanapewa Nafasi]"(Zaburi 1:1-2).
- Badili Mfumo Wako Wa Maisha, Toka Katika Ile Njia Ikupelekayo Dhambini Upesi... Amua Kuishi Kwa Ajili Ya Kumpendeza Mungu Kuliko Yeyote Au Chochote... HII INAHITAJI KUBADILI MFUMO WAKO WA MAWAZO [CHANGE OF MIND]... "MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII, BALI MFANYWE UPYA KWA KUGEUZWA NIA ZENU, MPATE KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU YALIYO MEMA, YA KUPENDEZA NA MAKAMILIFU" (Warumi 12:2).
- Dumu Kwenye Maombi Na Ushirika Na Mungu... MAOMBI YATAKUINGIZA KWENYE UWEPO WA MUNGU, NENO LAKE LITAKUFANYA USHIRIKIANE NAYE..."TENA IPOKEENI CHAPEO YA WOKOVU, NA UPANGA WA ROHO AMBAO NI NENO LA MUNGU. KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE"(Waefeso 6:17-18).
Rumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”
Pesquisar
Categorias
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Leia Mais
Verse by verse explanation of Exodus 36
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 22 questions at the...
MAVAZI YA KIKAHABA NI MACHUKIZO KWA BWANA MUNGU WAKO.
MAVAZI YA KIKAHABA NI MACHUKIZO KWA BWANA MUNGU WAKO
MAISHA BAADA YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
Mtu anapozaliwa mara ya pili kwa kumkaribisha Bwana Yesu ndani ya maisha yake, huingia katika...
BIBLIA NA MATULIZO YA MAPENZI
Kumekuwepo na kesi nyingi za wanandoa; kuvunjika kwa ndoa ni jambo la kawaida sana, watu...
Verse by verse explanation of Job 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...