Kwanini Mungu Hakumuua Nyoka, Akamwacha Hawa Ajaribiwe Katika Bustani Ya Edeni?

0
6K

JIBU: Hili ni swali watu wengi wanajiuliza ni Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, badala yake akamwacha Hawa ajaribiwe na yeye?.

Tunapaswa tufahamu wakati mwingine Mungu anaruhusu sisi wanadamu tujaribiwe kwa makusudi maalumu ili tuujue uweza wake na asili yake kwetu sisi na pia tumjue yeye zaidi, kwamfano jaribu kufikiria tungemjuaje kama yeye ni mwokozi kama tusingepotea katika dhambi?, tungejuaje yeye ni mponyaji kama tusingeumwa, tungejuaje yeye ni wa rehema kama tusingeanguka, tungejuaje yeye ni wa neema kama tusingekuwa hatuna haki, tungejuaje yeye ni mwenye msamaha kama tusingekuwa na makosa n.k…

Kumbuka pia sikuzote dhahabu ili ing’ae lazima ipitishwe kwenye moto mkali ijaribiwe na sisi kama watoto wa Mungu ni lazima tujaribiwe na ndio maana Mungu hakumuua shetani. Hata tulipokuwa shuleni, lengo la mwalimu kututungia mitihani migumu sio kutufunya sisi tufeli, hapana bali ni kutuimarisha zaidi ili tuweze kukabiliana na changamoto za mbeleni. Na ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni.   Mungu ana makusudi makubwa sana na sisi chini ya jua na ndio maana anatupitisha katika njia hiyo. Tunachopaswa kufahamu ni kuwa siku zote Mungu anatuwazia mawazo yaliyo mema  

Yeremia 29:11 ” Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”  

Yote haya Mungu kayaruhusu ili kutuwekea msingi mzuri wa maisha yajayo matamu ya umilele yasiyokuwa na mwisho.   Hiyo ndio sababu kwanini Mungu hakumuua nyoka mwanzoni kabisa pale Edeni kabla hajaasi.

Zaburi 103:12 “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. 13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. 14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. 15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo”.

 

Ubarikiwe sana.


Pesquisar
Categorias
Leia Mais
ESTHER
Verse by verse explanation of Esther 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:49:39 0 5K
HOLY BIBLE
Jesus is God
"You are my witnesses," declares the LORD, "and my servant whom I have chosen, so that you...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 05:48:17 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?
Kabla ya kufahamu ubatizo ni nini…Hebu jiulize mtu katokea na akakuuliza “kuzamisha...
Por GOSPEL PREACHER 2022-03-29 23:48:26 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
TAMBUA NAFASI YAKO ULIOITIWA
Nafasi mbili za mkristo katika wokovu
Por Martin Laizer 2023-09-28 05:37:50 0 5K
OTHERS
MIJADALA YA DINI NI MUHIMU.
Watu wengi katika jamii yetu wanasema kuwa tusiendekeze mijadala ya dini. Wanasema kuwa ni tishio...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:14:33 0 5K