NANI ALIYE TOLEWA KAFARA, ISHMAEL AU ISAKA?
Сообщение 2021-12-24 22:41:15
0
5Кб
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni Ishmael, siyo Isaka, kama ambavyo Waislam wanadai? Vinginevyo, inawezekanaje Isaka awe "mtoto pekee wa kiume" wa Abram?
Jibu: Ni Isaka aliyetolewa kafara na si Ishmael kwa sababu angalau nne:
Hata Kurani haisemi kuwa alikuwa ni Ishmael: Mwanzo 22:2 inasema alikuwa ni Isaka. Kwa Waislam, ingawa Kurani ya kiislam inazungumzia jambo hili kwenye Sura 37:99-111, hakuna sehemu yoyote kwenye Kurani nzima inayosema kuwa huenda alikuwa Ishmael au Isaka. Kwa hakika, wanazuoni wengi wa awali wa kiislam walifundisha kuwa alikuwa ni Isaka, wakati wengine walifundisha kuwa alikuwa ni Ishmael. Tazama al-Tabari juzuu ya 2 uk.68. al-Tabari juzuu ya 2 uk.82-97 inasema mabingwa 16 wa kiislam walisema kuwa ni Isaka wakati mabingwa 23 wa kiislam walisema kuwa ni Ishmael.
Abram alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume wakati ule: Ishmael alikuwa na miaka 14 wakati Isaka alipozaliwa. Hajiri na Ishamael walifukuzwa na kwenda sehemu nyingine Isaka alipoachishwa kunyonya kwenye Mwanzo 21:8-10. Abraham alijaribiwa "kwa muda mrefu" baada ya hapo kwenye Mwanzo 21:34, na "mtoto wa kiume" alikuwa kwenye meza ya kutolea kafara kwenye Mwanzo 22:12.
Mrithi pekee: Isaka alikuwa mirthi pekee, na mtoto pekee wa kiume, pia inamaanisha "mtoto wa kiume mpendwa". Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu watu kuwa na masuria kwa ajili ya kupata watoto, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza vilienda kwa watoto wa kiume wa mke halisi, siyo watoto wa kiume wa masuria. Tazama Mambo Magumu kwenye Biblia na Mambo Yanayoonekana Kupingana uk.141 kwa maelezo kamili.
Mwana pekee wa ahadi: Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utatajwa." Abraham alikuwa na watoto wengine pia wa kiume, lakini walizaliwa baada ya ahadi hii.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Поиск
Категории
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Больше
Is Baptism Necessary for Salvation?
One of the most nagging questions in Christianity is whether or not baptism is necessary...
MWANAMKE SIMAMA KWENYE NAFASI YAKO ILI UIPONYE NDOA YAKO
Namshukuru Mungu ambaye anazidi kunipa neema ya kuandika na kuandika masomo mbalimbali na pia...
YESU NI MWANA WA MUNGU MAANA YAKE NINI?
Wanadhuoni wa Kiislam pamoja na waumini wa dini ya Kiislam huwa wanauliza na kusema kwa Wakristo...
Allah is never found in the Bible
I. Allah is never found in the BibleContrary to Muslim claims, the word "Allah" is never...
The Holy Spirit In The Life Of Christ
In Luke 1:35 the angel Gabriel announces to Mary, “The Holy Spirit will come upon...