NANI ALIYE TOLEWA KAFARA, ISHMAEL AU ISAKA?
Veröffentlicht 2021-12-24 22:41:15
0
5KB
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni Ishmael, siyo Isaka, kama ambavyo Waislam wanadai? Vinginevyo, inawezekanaje Isaka awe "mtoto pekee wa kiume" wa Abram?
Jibu: Ni Isaka aliyetolewa kafara na si Ishmael kwa sababu angalau nne:
Hata Kurani haisemi kuwa alikuwa ni Ishmael: Mwanzo 22:2 inasema alikuwa ni Isaka. Kwa Waislam, ingawa Kurani ya kiislam inazungumzia jambo hili kwenye Sura 37:99-111, hakuna sehemu yoyote kwenye Kurani nzima inayosema kuwa huenda alikuwa Ishmael au Isaka. Kwa hakika, wanazuoni wengi wa awali wa kiislam walifundisha kuwa alikuwa ni Isaka, wakati wengine walifundisha kuwa alikuwa ni Ishmael. Tazama al-Tabari juzuu ya 2 uk.68. al-Tabari juzuu ya 2 uk.82-97 inasema mabingwa 16 wa kiislam walisema kuwa ni Isaka wakati mabingwa 23 wa kiislam walisema kuwa ni Ishmael.
Abram alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume wakati ule: Ishmael alikuwa na miaka 14 wakati Isaka alipozaliwa. Hajiri na Ishamael walifukuzwa na kwenda sehemu nyingine Isaka alipoachishwa kunyonya kwenye Mwanzo 21:8-10. Abraham alijaribiwa "kwa muda mrefu" baada ya hapo kwenye Mwanzo 21:34, na "mtoto wa kiume" alikuwa kwenye meza ya kutolea kafara kwenye Mwanzo 22:12.
Mrithi pekee: Isaka alikuwa mirthi pekee, na mtoto pekee wa kiume, pia inamaanisha "mtoto wa kiume mpendwa". Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu watu kuwa na masuria kwa ajili ya kupata watoto, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza vilienda kwa watoto wa kiume wa mke halisi, siyo watoto wa kiume wa masuria. Tazama Mambo Magumu kwenye Biblia na Mambo Yanayoonekana Kupingana uk.141 kwa maelezo kamili.
Mwana pekee wa ahadi: Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utatajwa." Abraham alikuwa na watoto wengine pia wa kiume, lakini walizaliwa baada ya ahadi hii.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Suche
Kategorien
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Mehr lesen
UTATU UNATHIBITISHWA KWA KUTUMIA HESABU/HISABATI
Kumekuwa na madai na hoja nyingi sana kuhusu hili swala la UTATU. Wengine wanasema kuwa...
JINSI YA KULINDA MOYO WAKO
Mithali 4;23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi...
JINSI SADAKA ZA WANA WA MUNGU ZINAVYOIBIWA WAKIFIKIRI WANAMTOLEA MUNGU NA KUMBE WAMEIBIWA PESA ZAO NA WATUMISHI.
BWANA YESU ASIFIWE. YESU WA NAZARETI aliye hai, tena anawapenda watu wote wabarikiwe kupitia njia...
Can I become a disciple of Christ?
You certainly can become a disciple of Christ. Discipleship is not just aimed at pastors and...
KUPENDANA HUSITIRI DHAMBI
Ndugu zangu,
Nawasalimu katika jina la Yesu. Mungu mwema kwa neema zake leo tena tumepata neema...