FAHAMU UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO

0
6χλμ.

Ukweli ni kwamba katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-

  1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu cha 1Yohana 1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

 

  1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”

 

  1. Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 6:53-54 kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE…..”

 

  1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; “Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya mwana-Kondoo….” Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu. Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako unaposoma na ketenda neno lake.

 

Αναζήτηση
Κατηγορίες
Διαβάζω περισσότερα
Injili Ya Yesu Kristo
YESU KRISTO AMEKUPA UTAJIRI
Watu wengu wanafikiri kuwa, Mungu aliwaumba ili wawe watu wa kawaida tu, la hasha, Mungu...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:27:06 0 5χλμ.
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
What is a Tithe?
What does the Bible say about tithing Tithing is the practice of setting aside 10% of your...
από BIBLICAL FINANCES 2021-12-29 14:51:07 0 7χλμ.
Injili Ya Yesu Kristo
TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
από GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:35:38 2 5χλμ.
OTHERS
Je Korani inawasifia Wakristo?
Wakristo wamo ndani ya Korani, na mara nyingi wanaitwa “Watu wa Kitabu kile” Huu ni...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:30:25 0 5χλμ.
MASWALI & MAJIBU
Ni nani anayetawala dunia kati ya Mungu na shetani?
Swali linaendelea….Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama...
από GOSPEL PREACHER 2022-06-13 00:07:33 0 5χλμ.