FAHAMU UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO
Imetumwa 2021-12-24 06:24:49
0
6K
Ukweli ni kwamba katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-
- Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu cha 1Yohana 1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.
- Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”
- Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha Yohana 6:53-54 kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE…..”
- Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; “Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya mwana-Kondoo….” Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu. Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako unaposoma na ketenda neno lake.
Tafuta
Vitengo
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Soma Zaidi
What did Jesus come to do?
To reveal the Father (Matt. 11:27)
"All things have been committed to me by my Father. No...
Verse by verse explanation of Joshua 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
Verse by verse explanation of 2 Samuel 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
BIOLOGY: FORM 1
List of all topics in Biology for form 1 class: CLICK HERE TO DOWNLOAD.
INTRODUCTION TO BIOLOGY...
MAJIRA YA KANISA LA FILADELFIA
(1) MLENGWA WA KANISAUFUNUO 3:7“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia...