NINI MAANA YA MTU KUZIKWA NDANI YA KANISA? KATIKA NYUMBA YA IBADA?

0
5K

Ukisoma katika kitabu cha Mathayo 22:32 inasema mimi ni MUNGU wa Ibrahim, na MUNGU Isaka, na MUNGU wa Yakobo. MUNGU si MUNGU wa wafu, bali wa walio hai. Sisi sote ni kizazi cha Ibrahimu ambaye MUNGU wake ndiye aliyekuwa MUNGU wa walio hai yaani watu wenye uhai na siyo waliokufa. Sasa ninachofundisha hapa ni watu kuelewa ukweli wasipotee wakifikiri wanamwabudu MUNGU aliye hai bali inakuwa ni upofu wa macho pasipo watu kujua au kuelewa waliabudu mahali ambapo upo mzoga au mauti ndani ya kanisa. Inapokuwa mtu amezikwa ndani ya kanisa au kupeleka maiti yake au mifupa basi tayari madhabahu hiyo inakuwa ni ya mungu wa wafu ndiye atawalaye na watu wataongozwa na mungu mfu.

Ukisoma katika biblia baba yetu Ibrahimu mwenyewe aliyembarikiwa yeye hajazikwagwa ndani ya kanisa au hekalu, pia YESU mwenyewe mwana wa MUNGU maiti yake haikuzikwa kanisani alizikwa mbali sababu madhabahuni ni mahali patakatifu pa MUNGU aliye hai na yeye ndiye hukaa pale, na inapofanyika maiti inazikwa pale inabadilika mara moja anakuja kuishi mungu wa wafu, na ukisoma biblia utaona MUNGU amekataa yeye ni MUNGU aliye hai maiti izikwe pale iozee pale? Na zaidi ukisoma katika kitabu cha Marko 12: 27, neno linasema yeye si MUNGU wa wafu bali ni MUNGU wa walio hai. Hivyo  wapotea sana, maeneo haya aliyasema MUNGU ya kuwa mwapotea sana yaani kupita kiasi na bila kujua katika ulimwengu huu. Ndiye sababu hataki  ibada za wafu ila leo zipo na kama zipo zinafanywa basi waelewe wafanyao hayo wao wapo chini ya mungu mfu. Sasa ni wakati wa kumrejea MUNGU wa kweli na siyo mungu wa wafu. Na wewe unayependa kuwa chini ya MUNGU wa uhai inakupasa kujitenge na mambo ya wafu na hata kuzikiwa vitu au makaburi kujengwa kanisani au katika madhabahu, inapokuwa ni hivyo basi hapo shetani anapata nafasi ya kuwateka watu wale sababu tu ya wafu

Kila mtu anajua ukisoma Marko 11: 15-18 hata YESU alipoingia katika hekalu alikuta waliofanya mambo ya biashara, alijua tayari MUNGU siyo mahali pake tena hivyo ili pawe na MUNGU aliye hai aliviondoa na kuwafukuza hekalu likabaki safi na MUNGU akatukuzwa. Na zaidi hata kibinadamu mtu ukikaa karibu na kaburi unaogopa linatisha, sababu katika kaburi inaishi roho ya mauti na ikiwa ni hivyo basi uelewe na madhabahu hizo zinaishi roho za mauti na mahali palipo na mauti anaishi mungu wa wafu. Hivyo unapoona hivyo uelewe ni mahali pa mungu wa wafu asiye na uhai na wanaoabudu hapo watashikiliwa na mungu mfu sababu anacho kibali, mahali unaposali ndipo na baraka za maisha yako yaliopo. Ikiwa kuna uzima utapata uzima, ikiwa kuna wafu utapata umaiti na kuhukumiwa usiende mbinguni.

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
Injili Ya Yesu Kristo
DALILI ZA KUMJUA MTUMISHI/NABII WA UONGO.
Ndugu msomaji na mwanadamu uliyeumbwa kwa mfano wa sura ya MUNGU na siyo ya shetani, MUNGU huyu...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:52:58 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
IMENIPASA KUWAMO KATIKA NYUMBA YA BABA YANGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:49:42 0 6K
STANDARD 1
STANDARD 1
List of all subjects for the standard 1 class
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:18:32 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU
“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:09:17 0 6K
SPIRITUAL EDUCATION
IT IS NOT FOR THE ANOINTED
This message was given to me on the evening of  March 29, 2014 in Njombe Region after...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:40:43 0 5K