KANUNI YA MUDA KATIKA MAHUSIANO

0
5KB

Muda hupima upendo wangu kwako.
Kama kweli nakupenda, nita tumia kiasi kikubwa cha Muda wangu kwa ajili yako! Kama nakunyima Muda wangu kila siku ni kwa sababu tu sikupendi. Inawezekanaje nikawa nakupenda wakati sina Muda na wewe? Muda ndiyo maisha yangu. Ninapotoa Muda wangu ninayatoa maisha yangu. Kwa nini? Maisha ya mtu yamefungwa ktk Muda wake, Muda wa mtu unajenga maisha yake.

Sasa ninapozungumzia Muda ninamaanisha Muda kwa ajili yake na si kwa ajili yako. Kama unatafuta Muda wa kuwa naye kwa ajili ya kutimiza matakwa yako na si kwa ajili yake (mwenzi wako) basi huo si dhabihu itakayojenga mahusiano yenu. Toa Muda wako kwa ajili ya Furaha yake kwanza. Furaha yake ndiyo Furaha yako. Kwanza yeye kisha wewe. Mpe Muda wako, Mpe maisha yako. Unaposhiriki Muda wako na umpendaye unashiriki maisha yako na umpendaye

UPENDO ni gharama, na gharama Inaanza na Muda wako kwa ajili yake. Ukiona huwezi kuutoa Muda wako kwa ajili yake jua umeshindwa kumpenda! Unayempenda utashiri naye Muda wako.

NINASHIRIKI VIPI MUDA WANGU NA MWENZI WANGU?

  1. Tumia Muda wako kumjulia hali na maendeleo yake; ukiwa mbali tumia simu yako, ukiwa karibu kaa naye, taka kujua taarifa zake alipokuwa mbali na wewe. Usiwe na haraka ya kuondoka wala usiwe bize na kitu kingine. Mwangalie usoni unapozungumza naye.
  2. Msikilize, onyesha unajali anachozungumza, onyesha kuwa unamsikia kwa kutikisa kichwa au kuitikia na Umwangalie anapokuwa anazungumza, kwa wanandoa unaweza kuwa umemshika au kumkumbatia wakati anapokuwa anazungumza au waweza kumlalia kifuani, begani au mapajani.
  3. Kula naye matunda ya kazi yako; Mpe sehemu ya unachopata kazini! Mletee zawadi itokanayo na matunda ya kazi yako.
  4. Kula naye chakula, ndani na nje ya nyumbani. Kama unauwezo wa kutoka 'out' na mwenzi wako si kwa sababu kuna kitu unakihitaji toka kwakwe bali kwa sababu unampenda na unataka afurahi basi mtoe
  5. Msifie, mfariji na umtie moyo. Kama kuna jambo la kumshukuru, basi, mshukuru kwa namna maalumu na kama kuna jambo ulimkosea basi maombi msamaha kwa uaminifu na unyenyekevu wote.


Fanya yote kana kwamba hautapata fursa nyingine tena, ni dhabihu ya maisha yako kwa mwenzi wako wa pekee asiye na mbadala

Pesquisar
Categorias
Leia mais
Injili Ya Yesu Kristo
NIMEKUTANA NA YESU KRISTO.
Mwaka 2012 mwezi Novemba, Nilikuwa mgonjwa sana na wazazi wangu wakanichukua na kunipeleka...
Por GOSPEL PREACHER 2022-07-10 05:31:42 0 7KB
MAHUSIANO KIBIBLIA
MAKOSA WANAYOFANYA VIJANA KATIKA KUTAFUTA MWENZI WA MAISHA.
KWA NINI VIJANA WENGI WANAKOSEA KATIKA KUTAFUTA MWENZI WA MAISHA? Maamuzi ya kuoa au kuolewa, si...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:27:24 0 7KB
NDOA KIBIBLIA
UNYETI NA UZITO WA NDOA
Shalom mpendwa,Leo ktk kona yetu hii nataka tuangalie unyeti na uzito wa ndoa kutokea ktk...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-06 13:10:52 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Hekima yao ikapate kuwa ubatili na maarifa yao yawe ujinga!
2Samuel 15:30-31 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia...
Por GOSPEL PREACHER 2022-04-01 09:26:31 4 7KB
DANIEL
DANIELI 9
Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe; Katika sura hii tunaona...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-08 01:31:39 0 9KB