JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

5
2K

*Je! sisi ni wafalme na makuhani kwa namna gani?*

 

Na: Martin Laizer

 

SWALI: Yohana hapa anasema Bwana ametufanya kuwa Ufalme na Makuhani Ufunuo1:6 …(Sasa hapa anamaanisha sasa hivi sisi ni wafalme na makuhani au ni katika ule umilele ujao?) na je! ni sahihi kumuita mwanamke kuhani??

 

JIBU: Ndio sasahivi sisi ni ufalme na makuhani wa Bwana katika roho,..kama vile Bwana Yesu alivyokuwa duniani tangu siku za kuzaliwa kwake mpaka siku za kuondoka kwake,,…tayari yeye alishakuwa mfalme,..Kama unakumbuka wale Mamajusi walimuuliza Herode yuko wapi mfalme wa wayahudi tunataka kumsujudia (Mathayo 2:3)? unaona hapo tangu alipokuwa mdogo tayari ni mfalme, pia Pilato tunaona baadaye siku chache kabla ya kuondoka kwake duniani alikuja kumuuliza Bwana …

 

Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?

 

34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?

 

35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?

 

36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.

 

37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.

 

Kwahiyo hata sisi tuliookolewa, na kuoshwa kwa damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, ni makuhani na ufalme. Lakini mambo hayo yatakuja kudhihirika katika ulimwengu unaokuja kama Bwana alivyosema ufalme wake ni wa ulimwengu unaokuja!…Na ukuhani wenyewe hautakuwa wa kuvukiza uvumba tena, ule ulikuwa ni taswira ya mambo yatakayokuja yanayofunua kumkaribia Mungu.. 

 

Vivyo hivyo na katika huo ulimwengu unaokuja hatutakuwa tu wafalme bali tutakuwa na uwezo kumkaribia Mungu kwa namna ya kipekee mfano wa makuhani, ambao sio watu wote watapewa uwezo huo bali ni wale watakaoshinda tu!.. Na thawabu hiyo itakuwa ni kwa wote…wanawake na wanaume.

 

Hivyo ukuhani wako mbele za Mungu unautengeneza ukiwa hapa hapa duniani, kwahiyo tunapaswa tukaze mwendo ili tusikose thawabu hizo.

 

Ubarikiwe sana.

Cerca
Categorie
Leggi tutto
Injili Ya Yesu Kristo
UNYAKUO NI NINI NA NI LINI? KINA NANI WATANYAKULIWA?
JE UNAO UHAKIKA UTANYAKULIWA NA YESU KWENDA MBINGUNI AU UTAACHWA HAPA DUNIANI? BWANA YESU...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:42:06 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
If Jesus is God, then who did He pray to?
This is a very common question and the answer is found in understanding...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:03:16 0 5K
OTHERS
WAISLAM WANASEMA KUWA WACHUNGAJI NI MBWA
1. Je Allah wa Quran ni Mchungaji?2. Je, Nabii Muhammad ni Mchungaji?   Naanza na mbwembwe...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:17:02 0 5K
MAHUSIANO KIBIBLIA
ZINGATIA YAFUATAYO ILI KUANZISHA MAHUSIANO SAHIHI YANAYOFIKIA MALENGO
UTANGULIZIMahusiano sahihi ni mahusiano ya namna gani?Mahusiano sahihi ni mahusiano yale ambapo...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:04:31 0 8K
Networking
How to launch your marketplace
It is time to put your marketplace to its first true test: can you facilitate transactions...
By Business Academy 2022-09-17 04:06:13 0 9K