JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

5
2KB

*Je! sisi ni wafalme na makuhani kwa namna gani?*

 

Na: Martin Laizer

 

SWALI: Yohana hapa anasema Bwana ametufanya kuwa Ufalme na Makuhani Ufunuo1:6 …(Sasa hapa anamaanisha sasa hivi sisi ni wafalme na makuhani au ni katika ule umilele ujao?) na je! ni sahihi kumuita mwanamke kuhani??

 

JIBU: Ndio sasahivi sisi ni ufalme na makuhani wa Bwana katika roho,..kama vile Bwana Yesu alivyokuwa duniani tangu siku za kuzaliwa kwake mpaka siku za kuondoka kwake,,…tayari yeye alishakuwa mfalme,..Kama unakumbuka wale Mamajusi walimuuliza Herode yuko wapi mfalme wa wayahudi tunataka kumsujudia (Mathayo 2:3)? unaona hapo tangu alipokuwa mdogo tayari ni mfalme, pia Pilato tunaona baadaye siku chache kabla ya kuondoka kwake duniani alikuja kumuuliza Bwana …

 

Yohana 18: 33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?

 

34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?

 

35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?

 

36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.

 

37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”.

 

Kwahiyo hata sisi tuliookolewa, na kuoshwa kwa damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, ni makuhani na ufalme. Lakini mambo hayo yatakuja kudhihirika katika ulimwengu unaokuja kama Bwana alivyosema ufalme wake ni wa ulimwengu unaokuja!…Na ukuhani wenyewe hautakuwa wa kuvukiza uvumba tena, ule ulikuwa ni taswira ya mambo yatakayokuja yanayofunua kumkaribia Mungu.. 

 

Vivyo hivyo na katika huo ulimwengu unaokuja hatutakuwa tu wafalme bali tutakuwa na uwezo kumkaribia Mungu kwa namna ya kipekee mfano wa makuhani, ambao sio watu wote watapewa uwezo huo bali ni wale watakaoshinda tu!.. Na thawabu hiyo itakuwa ni kwa wote…wanawake na wanaume.

 

Hivyo ukuhani wako mbele za Mungu unautengeneza ukiwa hapa hapa duniani, kwahiyo tunapaswa tukaze mwendo ili tusikose thawabu hizo.

 

Ubarikiwe sana.

Rechercher
Catégories
Lire la suite
SPIRITUAL EDUCATION
JINSI LAANA YA ROHO MTAKATIFU INAVYOENDELEA MIONGONI MWA WAHUBIRI WA INJILI PASIPO KUJIJUA.
JINSI LAANA YA ROHO MTAKATIFU INAVYOENDELEA MIONGONI MWA WAHUBIRI WA INJILI PASIPO KUJIJUA.
Par Martin Laizer 2024-01-06 17:28:15 0 7KB
UCHUMBA KIBIBLIA
WACHUMBA 7 WATAKAOSHINDWA
Kutahadharishwa mabaya ni kutayarishwa kwa mazuri“Ni yale mambo...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-06 11:03:29 0 5KB
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
Par THE HOLY BIBLE 2022-01-24 09:44:08 0 5KB
OTHERS
MUHAMMAD ALIKUWA NA WAKE ZAIDI YA 20
Huu ni MSIBA mkubwa sana. Ifuatayo ni orodha ya wake wa Muhammad iliyoandaliwa na mwanazuoni wa...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:48:32 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
HAKIMU ALIYE TOFAUTI NA MAHAKIMU WOTE
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary...
Par GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:34:25 0 5KB