KUPENDANA HUSITIRI DHAMBI

0
6KB
Ndugu zangu,
Nawasalimu katika jina la Yesu. Mungu mwema kwa neema zake leo tena tumepata neema ya kumtumikia. 
Napenda tumtafakari Mungu kwa maneno haya machache. Mtume Petro anasema "Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi" - 1 Petro 4:8
 
Kuna msemo wa kiswahili wanasema 'kupenda ni upofu'! Wanasema unapompenda mtu hata zile kasoro ambazo wengine wanaziona kwa huyo umpendae basi wewe huzioni. Sababu ni moja tu, Upendo husitiri dhambi wana wa Mungu.  Na mtume Petro anatukumbusha tuwe na bidii katika kupendana. Ndugu zangu tukiwa na bidii katika kupendana ndani ya jamii zetu, ndani ya madhehebu yetu, ndani ya ofisi zetu, ndani ya maeneo yetu tunayofanyia kazi, ndani ya mashambani mwetu, nakuambia katika jina la Yesu hutaona tofauti unazoziona kwa jirani yako au ndugu yako kama unavyoziona sasa. Lakini kwa sababu tu hatujatia bidii katika kupendana ndo maana tunaona hivi vitofauti vidogo vidogo hadi vinaibukia kututenganisha na kutufarakanisha.
 
Mwandishi wa Mithali 10:12 anasema "Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote"!.  Ndani ya ndoa zetu kumbe tukipendana viji-ugomvi visivyo na kichwa wala miguu hatutaviona wapendwa wana wa Mungu kwa sababu kuchukiana ndiko kunakoleta fitina. Tena "Upendo huvumilia" - 1Kor 13:4 ndio maana unakuwa kipofu kwa udhaifu kwa mwenzio.
 
Ndugu yangu ni ombi langu siku ya leo Roho Mtakatifu akusaidie uwe na bidii katika kupendana. Kwa maana kupendana kunasitiri dhambi mtumishi wa Mungu nakuambia. Inawezekana ndugu yako au jamaa yako au rafiki yako amekukosea au amekuwa akikukosea mara kwa mara ndo maana hutaki tena kumpenda. Lakini laiti Mungu angehesabu makosa yetu nadhani dunia hii tungekuwa tunapukutika kila siku. Basi nakuombea Roho Mtakatifu arudishe upendo wako wa kwanza na sasa uendelee mbele katika kupendana na jirani yako, na ndugu yako na rafiki yako. Mwambie Roho wa Mungu akusidie kupendana. Kwa nguvu zetu hatuwezi. Hebu omba neema ya Mungu katika hili.
 
Mungu akubariki sana.
Like
1
Pesquisar
Categorias
Leia mais
Injili Ya Yesu Kristo
MAFUNDISHO YA MASHETANI
1 Timotheo 4 : 1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine...
Por GOSPEL PREACHER 2022-06-04 16:00:49 0 5KB
OTHERS
KAMA YESU ALIKUWA NI MUNGU, JE ALIKUWA ANAMWOMBA NANI?
Swali la Yesu ni Mungu na nani alikuwa anamwomba, huwa linaleta utatanishi mkubwa sana na kama...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:39:43 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
YESU NI PENDO
Shetani anataka tuamini nini kuhusu jinsi Yesu anavyotuona, lakini Yesu anatuhakikishia nini?...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:33:08 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Por GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:33:56 0 5KB
HOLY BIBLE
Is Hell literally a place of fire and brimstone?
By raining down fire and brimstone upon the cities of Sodom and Gomorrah, God not only...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:19:42 0 6KB