Nawasalimu katika jina la Yesu. Mungu mwema kwa neema zake leo tena tumepata neema ya kumtumikia.
Napenda tumtafakari Mungu kwa maneno haya machache. Mtume Petro anasema "Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi" - 1 Petro 4:8
KUPENDANA HUSITIRI DHAMBI
Imetumwa 2021-09-24 08:13:26
0
6K

Ndugu zangu,
Kuna msemo wa kiswahili wanasema 'kupenda ni upofu'! Wanasema unapompenda mtu hata zile kasoro ambazo wengine wanaziona kwa huyo umpendae basi wewe huzioni. Sababu ni moja tu, Upendo husitiri dhambi wana wa Mungu. Na mtume Petro anatukumbusha tuwe na bidii katika kupendana. Ndugu zangu tukiwa na bidii katika kupendana ndani ya jamii zetu, ndani ya madhehebu yetu, ndani ya ofisi zetu, ndani ya maeneo yetu tunayofanyia kazi, ndani ya mashambani mwetu, nakuambia katika jina la Yesu hutaona tofauti unazoziona kwa jirani yako au ndugu yako kama unavyoziona sasa. Lakini kwa sababu tu hatujatia bidii katika kupendana ndo maana tunaona hivi vitofauti vidogo vidogo hadi vinaibukia kututenganisha na kutufarakanisha.
Mwandishi wa Mithali 10:12 anasema "Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote"!. Ndani ya ndoa zetu kumbe tukipendana viji-ugomvi visivyo na kichwa wala miguu hatutaviona wapendwa wana wa Mungu kwa sababu kuchukiana ndiko kunakoleta fitina. Tena "Upendo huvumilia" - 1Kor 13:4 ndio maana unakuwa kipofu kwa udhaifu kwa mwenzio.
Ndugu yangu ni ombi langu siku ya leo Roho Mtakatifu akusaidie uwe na bidii katika kupendana. Kwa maana kupendana kunasitiri dhambi mtumishi wa Mungu nakuambia. Inawezekana ndugu yako au jamaa yako au rafiki yako amekukosea au amekuwa akikukosea mara kwa mara ndo maana hutaki tena kumpenda. Lakini laiti Mungu angehesabu makosa yetu nadhani dunia hii tungekuwa tunapukutika kila siku. Basi nakuombea Roho Mtakatifu arudishe upendo wako wa kwanza na sasa uendelee mbele katika kupendana na jirani yako, na ndugu yako na rafiki yako. Mwambie Roho wa Mungu akusidie kupendana. Kwa nguvu zetu hatuwezi. Hebu omba neema ya Mungu katika hili.
Mungu akubariki sana.

Tafuta
Vitengo
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Soma Zaidi
Verse by verse explanation of Genesis 26
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 51 questions at the...
JIPANGE KABLA YA NDOA!
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi;
Moja ya tatizo kubwa linalowasumbua vijana ni...
JINSI YA KUISHINDA DHAMBI YA TAMAA ZA MWILI
WAGALATIA 5:16-17:-"Basi nasema, ENENDENI KWA ROHO, WALA HAMTAZITIMIZA KAMWE TAMAA ZA MWILI. Kwa...
Verse by verse explanation of Deuteronomy 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
UFUNUO 17
Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia...