Nawasalimu katika jina la Yesu. Mungu mwema kwa neema zake leo tena tumepata neema ya kumtumikia.
Napenda tumtafakari Mungu kwa maneno haya machache. Mtume Petro anasema "Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi" - 1 Petro 4:8
KUPENDANA HUSITIRI DHAMBI
نشر بتاريخ 2021-09-24 08:13:26
0
6كيلو بايت
Ndugu zangu,
Kuna msemo wa kiswahili wanasema 'kupenda ni upofu'! Wanasema unapompenda mtu hata zile kasoro ambazo wengine wanaziona kwa huyo umpendae basi wewe huzioni. Sababu ni moja tu, Upendo husitiri dhambi wana wa Mungu. Na mtume Petro anatukumbusha tuwe na bidii katika kupendana. Ndugu zangu tukiwa na bidii katika kupendana ndani ya jamii zetu, ndani ya madhehebu yetu, ndani ya ofisi zetu, ndani ya maeneo yetu tunayofanyia kazi, ndani ya mashambani mwetu, nakuambia katika jina la Yesu hutaona tofauti unazoziona kwa jirani yako au ndugu yako kama unavyoziona sasa. Lakini kwa sababu tu hatujatia bidii katika kupendana ndo maana tunaona hivi vitofauti vidogo vidogo hadi vinaibukia kututenganisha na kutufarakanisha.
Mwandishi wa Mithali 10:12 anasema "Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote"!. Ndani ya ndoa zetu kumbe tukipendana viji-ugomvi visivyo na kichwa wala miguu hatutaviona wapendwa wana wa Mungu kwa sababu kuchukiana ndiko kunakoleta fitina. Tena "Upendo huvumilia" - 1Kor 13:4 ndio maana unakuwa kipofu kwa udhaifu kwa mwenzio.
Ndugu yangu ni ombi langu siku ya leo Roho Mtakatifu akusaidie uwe na bidii katika kupendana. Kwa maana kupendana kunasitiri dhambi mtumishi wa Mungu nakuambia. Inawezekana ndugu yako au jamaa yako au rafiki yako amekukosea au amekuwa akikukosea mara kwa mara ndo maana hutaki tena kumpenda. Lakini laiti Mungu angehesabu makosa yetu nadhani dunia hii tungekuwa tunapukutika kila siku. Basi nakuombea Roho Mtakatifu arudishe upendo wako wa kwanza na sasa uendelee mbele katika kupendana na jirani yako, na ndugu yako na rafiki yako. Mwambie Roho wa Mungu akusidie kupendana. Kwa nguvu zetu hatuwezi. Hebu omba neema ya Mungu katika hili.
Mungu akubariki sana.
البحث
الأقسام
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
إقرأ المزيد
Kwa nini imani ya Kikristo ni bora zaidi ya Kiislamu?
1. Utangulizi
Kuamini juu ya Mungu Mmoja, ni imani katika Uwepo wa Utendaji wa Mungu mmoja [1]....
Verse by verse explanation of Psalm 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
HATARI YA KUHUBIRI WENGINE LAKINI KUWA MKATALIWA – FUNGUO LA YOHANA 4:23
Andiko Kuu: Yohana 4:23 – “Lakini wakati unakuja, na upo sasa, hapo...
NANI ALIYE TOLEWA KAFARA, ISHMAEL AU ISAKA?
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni...
KIPI KINAHITAJI MAANDALIZI SANA KATI YA NDOA NA HARUSI?
Shalom mpendwa wangu katika Kristo Yesu, Leo katika kona yetu hii ya mahusiano ya uchumba na...