Ni Sahihi Kumuita Mariamu Mama Wa Mungu?

0
7K

Kwa kuwa Bwana Yesu alipitia katika tumbo la Mariamu je! Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

JIBU: Mariamu alimzaa BWANA kwa namna ya mwili, hivyo wakati Bwana alipokuwa duniani ndio Mariamu alijulikana kama mama wa Yesu, na sio mama wa Mungu. Bwana Yesu alipokuja hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili lakini hakuja kutafuta kuabudiwa na ndio maana hakuna sehemu yoyote alijiita yeye ni Mungu, zaidi sana alikuwa anawarudisha watu wamuabudu Baba.   Kumbuka Mungu alipouvaa mwili ilimpasa afananishwe na mwanadamu kwa namna zote, azaliwe, ale chakula, asikie maumivu, alie, aone huruma, n.k. kama mwanadamu mwingine yeyote, si ajabu kumuona akiwa na Baba au bibi, au babu au mjomba, lakini haimaanishi kuwa yeye (YESU) yupo chini ya hao wote hapana..

Biblia inatueleza vizuri juu ya jambo hilo tukisoma katika..

Mathayo 22:41 Bwana Yesu alizungumza maneno haya;  

“41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena”.

Unaona hapo? jibu litakuwa pia hivyo hivyo kwa Mariamu kwamba Yesu atakuwaje mwanawe na wakati bado ni Bwana wake? na yeye ni binti wa Mungu (Kwasababu kama Daudi alikuwa mkubwa kuliko Mariamu aliambiwa hivyo je! si zaidi yeye?).  

Hivyo sisi wote tunaomwamini YESU KRISTO mbele zake ni ndugu na dada, Na yeye akiwa kama Baba yetu. Kwahiyo ni muhimu tujue kutofautisha jinsi Mungu anavyotenda kazi katika ofisi zake tofauti, Mungu anapoonyesha unyenyekevu (kuzaliwa kibinadamu) haimaanishi kuwa mwanadamu yupo juu yake. Hapana anafanya hivyo kutuonyesha sisi njia bora kama watoto wake.  

Ubarikiwe sana.


Zoeken
Categorieën
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
THE SPIRIT OF TRUTH
John 14:16-17 is written “And I will ask the Father, and He will give you another...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:33:12 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
JEHANAMU YA MOTO IPO NA ITAFANYA KAZI SIKU YA HUKUMU KUU. MATHAYO 13:40-50
JEHANAMU YA MOTO IPO NA ITAFANYA KAZI SIKU YA HUKUMU KUU. MATHAYO 13:40-50
By Martin Laizer 2024-01-22 10:52:31 0 9K
OTHERS
JE, YESU ALITUMWA KWA ISRAEL PEKE YAKE?
Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:11:00 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
SIRI YA MUNGU
Shalom Mwana wa Mungu, karibu tujifunze biblia, chakula cha uzima, kitupacho afya rohoni, leo...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 10:57:25 0 6K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 23
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 57 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 18:06:43 0 6K