Nini Maana Ya Kusali Kwa Kupayuka Payuka?

0
6KB
Swali linaendelea…..Na Je, nisali kwa namna gani ili maombi yangu yasionekane kuwa ni ya kupayuka payuka mbele za Mungu?
 
JIBU: Mungu akubariki ndugu,Mathayo 6:7 Inasema:
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
 Sasa mstari huo ukiangalia kwenye tafsiri nyingine hilo neno “kupayuka-payuka” halimaanishi kama “kupaza sauti kwa nguvu,” kama watu wengi wanavyodhani, hapana bali linamaanisha “KURUDIA-RUDIA” maneno yale yale, Hilo la kupaza sauti kwa nguvu mstari wake ni ule wa juu yake kabla ya huu unaosema:
“Mathayo 6: 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Unaona, aina hii ya watu ndio wanaopenda kupaza sauti zao kwa nguvu kwa lengo la kuonekana na watu ndio hao wanaoonekana wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia. Watu wa namna hiyo Bwana anasema Wamekwisha kupata thawabu yao, Lakini pia kumbuka hilo halimaanishi watu wasiombe kwa kupaza sauti zao, hapana, biblia inasisitiza sana tupaze sauti zetu tumliliapo Mungu…Lakini sio kwa lengo la kujionyesha sisi tunajua kusali, au sisi ni wa kiroho sana. Vinginevyo tutakuwa tumeshapata thawabu zetu.
 
Lakini sasa kwa wale wanao payuka payuka mstari wao ndio huo unaofuata…
 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. “
Hivyo watu wanao rudia-rudia maneno, kwa mfano watu dini nyingine na watu wanaosali rozari na sala za bikira mariamu wanafahamu,huwa wanarudia rudia maneno yale yale kwa muda mrefu hata masaa na masaa wakidhani kuwa kwa kufanya vile Mungu atasikia dua zao. Hizo ni desturi za kipagani ndio maana tumeonywa tusifanane na hao. kwahiyo tunapoenda mbele za Mungu tuwe na malengo, tutoe hoja zetu zote, kisha zikishaisha, basi, tushukuru tuondoke Tukiamini kuwa Mungu kashatusikia na sio kuanza kurudia rudia tena kile tulichokiomba kana kwamba Mungu hasikii,. kwa ufupi usiweke mfumo fulani unaoonyesha mrudio rudio katika kusali, kuwa huru mbele za Mungu ndivyo Sala zako zitakavyokuwa na thamani mbele za Mungu.
 
Ubarikiwe sana.

 

Pesquisar
Categorias
Leia mais
OTHERS
Debit Voucher, Credit Voucher, and Transfer Voucher
Voucher is the supporting documents that accountants use as the summary to record into the...
Por PROSHABO ACCOUNTING 2022-03-29 20:47:16 0 10KB
Injili Ya Yesu Kristo
IPONYE NAFSI YAKO, EPUKA MANABII WA UONGO
Muhubiri/ Mtumishi yeyote aliyerudi nyuma na kusahau kusudi lake tayari anageuka kuwa nabii wa...
Por GOSPEL PREACHER 2023-06-17 23:43:15 0 8KB
Injili Ya Yesu Kristo
KUANDAA MAHUBIRI
Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi ataweza. Kueleza maana yamahubiri. Kueleza...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-06 08:55:11 0 9KB
SPIRITUAL EDUCATION
HAZINA YA MTU
PALIPO NA HAZINA YA MTU NDIPO NA MOYO WAKE UTAKAPOKUWA 
Por Martin Laizer 2023-09-25 06:09:55 0 18KB
SPIRITUAL EDUCATION
JEHOVAH'S WITNESSES: FALSE TEACHINGS
JEHOVAH'S WITNESSES: The Watchtower Society FALSE TEACHINGS "If they speak not according to...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 18:44:06 0 6KB