Epuka Fundisho la Uongo kuwa "Mara Baada ya Kuokolewa, Umeokolewa Daima"

0
8K

Mafundisho machache ya uwongo ni hatari zaidi kuliko madai ya Calvin ya “usalama wa milele” au “mara tu mtu atakapookolewa, anaokolewa daima.” Imani hii imeenea zaidi ya uwezo wa wasomi wa theolojia. "Baada ya kuokolewa, kuokolewa daima" ni kauli-mbiu maarufu kwa "mkristo mwenye uelewa wa chini". Kauli-mbiu hii inavuka mipaka ya kimadhehebu, kati ya wigo wa kitheolojia, na kuingia katika mafundisho ya kila siku.

Fundisho la usalama wa milele linasema kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwafanya watengwe na Mungu mara tu mtu anapookolewa. Bila kuingia ndani sana, ni lazima ieleweke kwamba kuna tofauti nyingi na mbinu za mafundisho haya. Katika imani hii, mtu anaweza akamuua mke wake huku akibaki "ameokoka na asihesabike kuwa na dhambi (maana wao eti wameokolewa milele). Ingawa wapo wengine wangedai kwamba ikiwa mtu angefanya kitendo kiovu kama hicho, basi mtu huyo hakuwahi kuokolewa “kikwelikweli” hapo kwanza.

Cha kusikitisha ni kwamba, fundisho hili hatari linapingana kabisa na Maandiko, na kwa kawaida hutumiwa kama nyenzo yao ili kuhalalisha maisha ya dhambi. Kwa maneno mengine, hii kauli-mbiu kuwa “mara tu baada ya kuokolewa, unakuwa umeokolewa daima” huvutia mielekeo ya kimwili zaidi ya ubinadamu wetu. Inatoa uhalali wa dhambi, faraja ya uwongo kwa wenye dhambi, na inajenga kizuizi kwa wenye dhambi kutubu, na ndilo hasa lengo la Shetani.

Mafundisho ya usalama wa milele yanapingana kabisa na Maandiko, na kwa kawaida hutumiwa kama nyenzo ya kuhalalisha maisha ya dhambi. Kwa maneno mengine, “mara tu baada ya kuokolewa, kuokolewa daima” huvutia mielekeo ya kimwili zaidi ya ubinadamu wetu.

Tweet
Fundisho la usalama wa milele linatoa uhalali wa uongo wa dhambi, faraja ya uongo kwa wenye dhambi, na kujenga kizuizi cha uwongo cha kibiblia kati ya wenye dhambi wengi na toba.

Tweet
Inashangaza jinsi wazo la Calvin la usalama wa milele linavyoshiriki kufanana na ulaghai wa Shetani wa Hawa katika bustani ya Edeni. Nyoka alimhakikishia Hawa, “…Hakika hamtakufa (Mwanzo 3:4).” Maana ya kishetani ni kwamba Hawa angeweza kuishi katika kutotii bila kuogopa matokeo ya Kimungu. Fundisho la usalama wa milele hufanya dai lile lile la uwongo, nalo linatoka katika chanzo kile kile cha kishetani. Hiki ndicho kifungu cha msingi cha Maandiko kinachotumika kuunga mkono wazo la kuokolewa mara moja, kuokolewa kila wakati:

Warumi 8:35-39; inasema 35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Fundisho la usalama wa milele linashiriki ufanano na ushawishi wa Shetani kwa Hawa katika bustani ya Edeni. Shetani akasema, Hakika hamtakufa. Maana yake ni kwamba Hawa angeweza kuishi katika kutotii bila kuogopa matokeo ya Kimungu.

Tweet

Kwanza kabisa, hiki ni kifungu cha Maandiko cha kutia moyo sana, lakini kinazungumza kuhusu upendo wa Mungu usio na masharti, na kamwe hakizungumzii wokovu usio na masharti. Ukichunguza kwa makini, utaona kwamba dhambi haijatajwa hata mara moja katika muktadha wa ahadi hii. Kama vile vifungu vingine vinavyotumiwa kuunga mkono O.S.A.S. (Yohana 3:15, Yohana 5:24, Yohana 10:28, Warumi 8:1, 1 Wakorintho 10:13), msisitizo daima ni juu ya nguvu za nje zisizo na mamlaka juu ya wajibu wako binafsi kwa Mungu.

Hebu tuweke hivi; hakuna kinachoweza kukulazimisha kujitenga na Mungu isipokuwa wewe. Shetani hawezi kukufanya ufanye zaidi ya vile alivyomfanya Hawa afanye. Hawa alitumia hiari yake. Adamu alitumia hiari yake. Na wote wawili walipata matokeo ya matendo yao. Dhambi hututenganisha/huvumja uhusiano wetu mzuri na Mungu, lakini haituondoi katika upendo wa Mungu. Kwa mfano, Biblia inasema “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. (Warumi 5:8). Mungu anatupenda hata tukiwa katika dhambi, lakini kusema kuwa msalaba unakupatia uhalali wa kufanya dhambi bila kupoteza wokovu, ni kudhoofisha kabisa ulazima wa msalaba. Maneno "tulipokuwa bado wenye dhambi" yanaonyesha dhana ya Paulo kwamba waumini wanapaswa kuelewa kuwa kuwa maisha ya dhambi ni lazima yatupiliwe mbali baada ya wokovu. Zaidi ya hayo, mtume Petro anatuita tufuate nyayo za Yesu, “Yeye hakutenda dhambi (1 Petro 2:21-22).” Mistari michache chini, yaani (1 Petro 2:24-25). inasisitiza kwamba Yesu “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu." 

Hakuna kinachoweza kukulazimisha kujitenga na Mungu isipokuwa wewe. Shetani hawezi kukufanya ufanye zaidi ya vile alivyomfanya Hawa afanye. Hawa alitumia hiari yake. Adamu alitumia hiari yake. Na wote wawili walipata matokeo ya matendo yao.

Mungu anatupenda hata tukiwa katika dhambi, lakini kusema msalaba uliofanya dhambi kukubalika ni kudhoofisha ulazima wa msalaba kwanza kabisa.

Lakini bado hatujakanusha vya kutosha fundisho hili potofu la usalama wa milele hata ukiendelea na maisha ya dhambi. Watu wachache wanaweza kubishana dhidi ya msisitizo wa Kimaandiko wa kuishi juu ya dhambi. Wengi wangesema kwamba kuishi kwa haki ndiyo njia bora zaidi lakini si hitaji la Mbinguni baada ya utii kwa Injili. Kwa hivyo, hebu tuangalie Maandiko kadhaa ambayo yanathibitisha kwamba inawezekana kutupa/kupoteza wokovu wetu na kukanyaga/kuidharau neema ya Mungu.

Mfano wa mpanzi hutusaidia kuelewa suala linalohusika. Yesu anazungumza juu ya watu binafsi wanaopokea Injili mara moja kwa furaha, lakini wakati dhiki au mateso yanapotokea kwa sababu ya Neno, wanaanguka (Marko 4:16, Luka 8:13).

Fikiria Maandiko haya yenye kujieleza kutoka katika kitabu cha Waebrania:

Waebrania 6:4-6 inasema kuwa "4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri."

Waebrania 10:26-27 inasema kuwa "26Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao."

Waebrania 10:38-39 inasema kuwa "38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. 39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu."

Zaidi ya hayo, Petro anazungumza waziwazi juu ya watu wanaorudi na “kushindwa” na “uchafu wa dunia,” akisema kwamba ingekuwa bora zaidi kama hawangejua kamwe “njia ya haki” hapo kwanza, hebu tusome 2 Petro 2:20-22, Biblia inasema "20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. 21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. 22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni."

Lakini maneno ya Yesu ndiyo yenye nguvu zaidi, katika ile Mathayo 7:21-23 ambapo Biblia inasema kuwa, "21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."

Tunaweza kuendelea na kuendelea kuonyesha sharti la Kimaandiko kwamba hatupaswi kuendelea na maisha ya dhambi baada ya kupokea wokovu vinginevyo tunajiweka kwenye hatari ya kupata hukumu ya Kiungu (hasa kama hatutatubu). Nitakuacha na orodha ya Maandiko yanayothibitisha kwamba watu waliookoka lazima waendelee “kuutimiza wokovu wao kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12).”

Ukweli ni huu, watoto wa Mungu wasipokaa vizuri katika wokovu wao basi wanaweza:

  1. "Kuanguka na kutoka kwenye neema" - Wagalatia 5:1-4,13
  2. “Kuchukuliwa na kosa na kuanguka.”— 2 Petro 3:17
  3. “Kupotelea mbali na kweli.”— Yakobo 5:19-20
  4. “Kuangamia hasa akiwa dhaifu.”— 1 Wakorintho 8:11
  5. “Kuangukia hukumuni.”— Yakobo 5:12
  6. “Kuondoshwa mbali na tumaini.”—Wakolosai 1:21-23
  7. "Kumkana Bwana Yesu aliyewanunua" - 2 Petro 2:1
  8. “Kwenda mbali na Mungu aliye hai.”— Waebrania 3:12
  9. “Kutupwa nje” - 1 Wakorintho 9:27
  10. “Wanaweza kuwa watoto waliolaaniwa.”— 2 Petro 2:14

MUNGU AKUBARIKI SANA

Love
1
Cerca
Categorie
Leggi tutto
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 36
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 02:39:04 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 35 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:15:30 0 5K
OTHERS
Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!
Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 20:19:52 0 5K
OTHERS
JE, YESU ALITUMWA KWA ISRAEL PEKE YAKE?
Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:11:00 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
ZIJUE FUMBO ZA ADUI SHETANI ILI ZISIKUNASE
Kati ya yale makanisa 7 tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Thiatira, lilikuwa ni la...
By GOSPEL PREACHER 2023-08-19 23:32:40 0 7K