Nini Maana Ya Kusali Kwa Kupayuka Payuka?

0
5K
Swali linaendelea…..Na Je, nisali kwa namna gani ili maombi yangu yasionekane kuwa ni ya kupayuka payuka mbele za Mungu?
 
JIBU: Mungu akubariki ndugu,Mathayo 6:7 Inasema:
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
 Sasa mstari huo ukiangalia kwenye tafsiri nyingine hilo neno “kupayuka-payuka” halimaanishi kama “kupaza sauti kwa nguvu,” kama watu wengi wanavyodhani, hapana bali linamaanisha “KURUDIA-RUDIA” maneno yale yale, Hilo la kupaza sauti kwa nguvu mstari wake ni ule wa juu yake kabla ya huu unaosema:
“Mathayo 6: 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Unaona, aina hii ya watu ndio wanaopenda kupaza sauti zao kwa nguvu kwa lengo la kuonekana na watu ndio hao wanaoonekana wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia. Watu wa namna hiyo Bwana anasema Wamekwisha kupata thawabu yao, Lakini pia kumbuka hilo halimaanishi watu wasiombe kwa kupaza sauti zao, hapana, biblia inasisitiza sana tupaze sauti zetu tumliliapo Mungu…Lakini sio kwa lengo la kujionyesha sisi tunajua kusali, au sisi ni wa kiroho sana. Vinginevyo tutakuwa tumeshapata thawabu zetu.
 
Lakini sasa kwa wale wanao payuka payuka mstari wao ndio huo unaofuata…
 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. “
Hivyo watu wanao rudia-rudia maneno, kwa mfano watu dini nyingine na watu wanaosali rozari na sala za bikira mariamu wanafahamu,huwa wanarudia rudia maneno yale yale kwa muda mrefu hata masaa na masaa wakidhani kuwa kwa kufanya vile Mungu atasikia dua zao. Hizo ni desturi za kipagani ndio maana tumeonywa tusifanane na hao. kwahiyo tunapoenda mbele za Mungu tuwe na malengo, tutoe hoja zetu zote, kisha zikishaisha, basi, tushukuru tuondoke Tukiamini kuwa Mungu kashatusikia na sio kuanza kurudia rudia tena kile tulichokiomba kana kwamba Mungu hasikii,. kwa ufupi usiweke mfumo fulani unaoonyesha mrudio rudio katika kusali, kuwa huru mbele za Mungu ndivyo Sala zako zitakavyokuwa na thamani mbele za Mungu.
 
Ubarikiwe sana.

 

Cerca
Categorie
Leggi tutto
Injili Ya Yesu Kristo
Alipita katikati yao Akaenda zake!
Luka 4:16-30 “Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:24:42 0 10K
OTHERS
KORAN HAIKUTEREMSHWA KUTOKA KWA ALLAH
Je, ungependa kuwafahamu waandishi wa Koran? Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:27:10 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Sabato Halisi Ni Lini, Je! Ni Jumapili Au Jumamosi?, Ni Siku Gani Itupasayo Kuabudu?
JIBU: Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:33:45 0 5K
OTHERS
MWANAMKE WA KIISLAM HANA HAKI MBELE YA MUMEWE
Leo nitawapa hadith kadhaa kuhusu Wanawake wa Kiislam na jinsi wanavyo onewa na Mtume...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:32:08 0 5K
OTHERS
KWANINI SULEIMAN ALIKUWA NA WAKE MIA SABA (700) NA MASURIA MIA TATU (300)?
Kwenye 1 WaFalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 21:03:13 0 5K