Je! ni sahihi kuning’iniza picha nyumbani mwako kama ya Yesu?

0
6KB

Swali linaendelea…maana imeandikwa kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. “

Sasa naomba kufahamu kufanya hivyo ni makosa?


JIBU: kwa kulijibu hili swali tumalizie kusoma mstari huo..

Kutoka 20:4-5″ Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”…

Sasa tunaona katika huo mstari wa tano msisitizo umewekwa pale katika neno “USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA”, lakini sio kwamba ukiweka picha yoyote kama ya Yesu nyumbani mwako ni vibaya hapana! unaweza kuweka picha yoyote upendayo ilimradi iwe ni njema,

Maana tukisema tusiweke picha yoyote basi hata tunaponing’iniza picha zetu wenyewe ukutani majumbani mwetu tunafanya vibaya kwasababu maandiko yanasema usijifanyie mfano wa kitu chochote sio tu kilicho juu mbinguni bali hata kilichopo chini duniani.

Unaona hapo msisitizo ni kwamba unapoweka picha yoyote au sanamu yoyote hupaswi kuiabudu wala kuisujudia kwa kufanya hivyo ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Lakini leo hii kuna baadhi ya watu,na dini na madhehebu yanaabudu sanamu za Yesu na bikira Mariamu au watakatifu waliokufa zamani za kale hao ni dhahiri kuwa wanamwabudu shetani aidha kwa kujua au kwa kutokujua.

Ikiwa wewe ni mkatoliki na unayo sanamu ya Yesu au sanamu ya bikira Maria nyumbani mwako, nashauri iondoe haraka sana, kwasababu dini hiyo inaahusisha ibada zao na sanamu, vinginevyo utamtia Mungu wivu na kujikuta umeenda Jehanamu.

Lakini kama picha ipo kwa ajili ya urembo au kwa ajili ya kufikisha tu ujumbe fulani katika mazingira yanayokuzunguka au nyumbani kwako, wala husujudii wala kuabudu basi hakuna shida yoyote. Zingatia tu hilo neno ”USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA’ kwasababu yeye ni Mungu mwenye wivu.

Biblia inasema;

1 Wakorintho 10:14

[14]Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
[15]Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.

Ubarikiwe sana.

Rechercher
Catégories
Lire la suite
SPIRITUAL EDUCATION
MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:24:21 0 5KB
MAHUSIANO KIBIBLIA
KANUNI YA MUDA KATIKA MAHUSIANO
Muda hupima upendo wangu kwako.Kama kweli nakupenda, nita tumia kiasi kikubwa cha Muda wangu kwa...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-06 15:03:16 0 5KB
Religion
Jinsi Shetani Anavyopofusha Fikra za Watu: Maandiko ya Biblia Yanayofafanua
Katika Biblia, Shetani anaelezewa kama roho mbaya ambaye anaweza kushawishi, kudanganya, na...
Par GOSPEL PREACHER 2025-09-28 05:02:20 0 2KB
REVELATION
UFUNUO 5
Shalom! Karibu katika mwendelezo mfupi wa uchambuzi wa kitabu cha ufunuo, kwa neema za Mungu...
Par GOSPEL PREACHER 2021-10-30 09:41:30 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
YESU NI PENDO
Shetani anataka tuamini nini kuhusu jinsi Yesu anavyotuona, lakini Yesu anatuhakikishia nini?...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:33:08 0 5KB