KAMA YESU NI MUNGU, KWANINI ALIKUFA?
Postado 2021-12-25 11:50:46
0
5K

JE, MUNGU ANAKUFA?
Hayo ni maswali ya Waislam kila siku, na kwenye hii mada nitayajibu.
SOMA: 1 Petro 3: 18 - 19 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
Neno la Mungu linasema kuwa MWILI WAKE NDIO ULIUWAWA BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA. Sasa hakuna kushangaa tena maana tufahamu ulio uwawa ni Mwili wake tu bali Roho yake haikuuwawa.
Maandiko yanasema kuwa MUNGU NI ROHO, sasa aliye UWAWA NI MWILI TU BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA
1 Timotheo 6:15-16 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina
Hii asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1, 14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya Pili katika Utatu Mtakatifu. Biblia inatuambia katika Waebrania 1 aya ya 3 kuwa: Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni. Hivyo basi, asilia hizi mbili za Yesu Kristo haziwezi kuchanganywa (Eutychianism), vile vile haziwezi kuwa pamoja na kuwa Mungu-Mtu (Monophysitism). Hizi asili mbili ni tofauti na zinajitemea na wakati huohuo ni moja katika Yesu (person of Jesus). Huu muungano unaitwa Hypostatic Union.
USHAHIDI ZAIDI WA ASILIA MBILI YA YESU
Mafundisho ya muungano wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini “Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai kuwa alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.
Mafundisho ya muungano wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini “Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai kuwa alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.
Moja ya Makosa makubwa sana yanayo fanywa na wasio Wakristo ni kushindwa kwao kuelewa kuwa Yesu alikuwa na ASILIA MBILI. Kwa mfano, Mashahidi wa Yehova wao wanamwangali Yesu kama Binadamu na kupuuza adhama zake za Umungu. Mara zote wao hutumia zile aya ambazo zinakiri Ubinadamu wa Yesu na kuzipambanisha na aya ambazo zinasema kuwa Yesu ni Mungu. Kwa upande mwingine, Masayantisti wa Kikristo wao hufanya kinyume chake. Wao wana angalia zaidi upande wa Yesu ni Mungu na kusahau kuwa, Yesu alikuwa Binadamu vile vile.
Kuna aya nyingine nyingi ambazo zinamshuhudia Yesu kuwa ni Mungu nazo ni
Yohana 10:30-33; 20:28; Wakolosai. 2:9; Wafilipi. 2:5-8; Waebrania 1:6-8; na 2 Petro. 1:1.
Ili kumwelewa Yesu vyema, basi kila mafundisho ambayo yanamuhusisha Yesu, hayana budi kuzumgumzia Yesu kama Mungu na Yesu kama Binadamu. Hizo asilia Mbili ni zake. Kumbe ndio maana Yesu katika Luka 2:52 inasema: Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. Na wakati huo huo alikuwa kila kitu “omniscient” Soma Yohana 21:17. Yesu ni Neno la Mungu aliye kuwa Mwili/Binadamu (Yohana 1:1, 14).
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
Pesquisar
Categorias
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Leia Mais
Verse by verse explanation of Job 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
IGVault Fast Way to Make Money in Burning Crusade Classic 2022
As you are making your way through World of Warcraft: The Burning Crusade, you are going to...
Verse by verse explanation of Psalm 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 19 questions at the...
HATARI YA KUPENDA NAFSI
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe ...
Verse by verse explanation of Leviticus 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 54 questions at the...