UBATIZO WA MAJI MENGI.

Na Mch.Madumla ( wa katikati mbele)
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi;
Miaka fulani nilipata neema ya kwenda Israeli;katika mwaka wa kwanza wa kwenda huko nilitamani kufika eneo moja liitwalo “mto Yordani” kwa lengo moja tu la kubatizwa kwa maji mengi katika eneo hilo kama vile alivyobatizwa Yesu mahali hapo. Ni kweli Bwana akatufanikisha kufika hapo,na siku ya kubatizwa ikawadia. Tukiwa tukisubiri kubatizwa na pasta mmoja hivi kutoka Rwanda,mchungaji huyo akaja na tulikuwa si wengi tuliobatizwa siku hiyo kwa upande wetu watanzania. Mchungaji huyo akasema machache kama dakika 10 hivi kisha tukaingia kubatizwa. Kusema ukweli hakuna mtu miongoni mwetu alielewa ipasavyo,kwa sababu hayakuwa mafundisho rasmi kwa kweli!!! Lakini kubatizwa tulibatizwa kwa maji mengi tena Yordani mahali sahihi sana. Sasa angalia;mahali palikuwa ni sahihi lakini mafundisho tuliyoyapata hayakuwa sahihi,hivyo hatuelewa ! Na kwa sababu hiyo tulitimiza kubatizwa kama kubatizwa lakini tuliondoka “wakavu” bila udhihirisho wowote wa nguvu za Mungu.
Kumbe! Ishu sio kubatizwa tu,ishu ni kuelewa kwanza ndipo uamini na hatimaye ubatizwe. Sasa nimekuwa mwalimu mzuri wa mambo haya,ninatamani na nawe uelewe kwa undani ili ukibatizwa upokee nguvu kikamilivu kutoka kwa Bwana. Nilipoelewa ilinibidi nibatizwe tena kwa maana sio dhambi wala makosa kurudia ubatizo ikiwa kama ulibatizwa nje ya ufahamu sahihi,au ikiwa ulibatizwa kwa maji machache! Lakini ebu tujiulize sote ; Nini hasa maana ya ubatizo ? Na ni kwa nini hasa tubatizwe? Kwani kuna tofauti gani kati ya ubatizo wa maji machache na maji mengi? Kwa nini urudie ubatizo ikiwa ulikwisha batizwa ulivyokuwa mchanga kwenye dini yako? Shida ipo wapi usipobatizwa? N.K Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na wengi,hata mimi nilikuwa nikijiuliza. Lakini kwa neema tutajifunza machache hapa,mengine utanipigia simu nikufundishe zaidi.;
- Ubatizo ni nini?
Kuna sherehe mbili katika kanisa la kikristo .Sherehe hizi huitwa “church ordinance” yaani maagizo muhimu kwa kanisa,ambapo kanisa limeagizwa kuyatekeleza mara kwa mara.
- Meza ya Bwana – (Luka 22:19-20,1 Wakorintho 11:23-25)
- Ubatizo -(Mathayo 28:19)
Neno hili “ubatizo” limetokana na neno la Kiyunani “ Baptizein” Au immerse/baptize lenye maana ya “zamisha ndani ya…( to dip)“. Ubatizo ni kuzamisha ndani ya…Hivyo Ubatizo ni agizo/sherehe ya kumzamisha mtu ndani ya maji mengi kama ishara ya kuuzika utu wa kale,kisha kuupata utu mpya ndani ya Kristo – Warumi 6:3-4
Ubatizo kabla ya Kristo.
Wayahudi wa mwanzo walikuwa wakiwabatiza wamataifa wale watakaojiunga na dini yao. Inaonesha kuwa ubatizo ulikuwepo muda mrefu na ulikuwa ni ubatizo wa maji mengi. Jamii ya awali ilihitaji kuwaingiza wapagani na mataifa ndani ya dini zao kwa kuwabatiza. Mtu kama Yohana mbatizaji,alikuwa ni mmoja wa mfano mzuri aliyebatiza kabla ya ubatizo wa Kikristo.
Ubatizo wa Yohana mbatizaji.
Yohana mbatizaji yeye alibatiza kwa maji mengi (Yoh.3:23) Na ubatizo wake ulilenda juu ya:
- Alibatiza Bethania ngambo ya Yordani (Yoh.1:28,3:23)
- Alibatiza watu wengi – Mathayo 3:5-6
- Alibatiza kwa ajili ya toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi – Matendo 13:24,Luka 3;3
- Kuwaandaa watu kumpokea Yesu -Luka 7;29-30,Yoh.1;23
- Kutangaza wazi juu ya wokovu pamoja na ghadhabu kali ya Mungu – Mathayo 3;12
Ubatizo wa Yohana mbatizaji ulikuwa ni kivuli cha ubatizo wa Kikristo,Yeye Yohana mbatizaji alionesha picha ya ubatizo utakavyokuwa kwanza kwa kubatiza kwa maji mengi lakini pia kuhusisha imani. ( Matendo 19:4-5 Andiko la muhimu sana linaloonesha ubatizo wa Yohana mbatizaji na ubatizo wa Kikristo)
Ubatizo wa Yesu (Wa Kikristo)
- Alibatizwa na Yohana mbatizaji (Mathayo 3:13-17)
- Alibatizwa kwa maji mengi -Mathayo 3:16 “…alipokwisha kubatizwa mara akapanda..”
- Utatu wote ulihusika
- Mungu alimtambulisha rasmi.
- Roho mtakatifu alishuka.
Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana mbatizaji,Je alitenda dhambi gani kwani? kama la hakutenda,kwa nini basi abatizwe?
- Kuitimiza haki yote.
- Kumtambulisha kuwa Yeye ni masihi wa Bwana.
- Kuweka mfano kwetu,kwamba lazima tubatizwe kwa maji mengi ndani yake.
Mifano michache yaonekana;
- Kuvuka kwa wana wa Israeli kwenye bahari ya shamu wakitokea utumwani Misri – 1 Wakorintho 10:1-2
- Kuelea kwa safina wakati wa Nuhu – 1 Petro 3;20-21
- Kutailiwa / Tohara – Wakolosai 2;11-12
Mifano ya ubatizo wa maji mengi katika agano jipya.
- Yesu kubatizwa na Yohana mbatizaji – Mathayo 3:15-16 ( Kwa maelezo zaidi katika eneo hili,utahitaji unipigie tuongee zaidi)
- Towashi wa kushi – Matendo 8:38
- Waliookoka wengi huko Samaria – Matendo 8:12 n.k
- Watu 3,000 kwenye Pentekoste -Matendo 2:41
- Waamini Samaria -Matendo 8:12
- Lydia na nyumba yake – Matendo 16:15
- Mlinzi wa gereza na nyumba yake -Matendo 16:33
- Waamini Korintho – Matendo 18:8
- Gayo,Krispo na nyumba ya stephana -1 Wakorintho 14:16
- Sauli (Paulo) – Matendo 9:18 n.k
Kusudi la ubatizo wa maji mengi. – Kuanza maisha mapya ndani ya Kristo kwa kuzaliwa upya.
Mambo ya kuzingatia;
- Ubatizo umeamliwa na Yesu mwenyewe,sio mapenzi ya mtu – Mathayo 28:19
- Mafundisho pamoja na mtumishi awepo.
- Maji mengi ni lazima – Matendo 8:37-38
- Ubatizo ufanywe kwa Jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu -( Mathayo 28:19). Ijapokuwa mitume walibatiza kwa jina la Yesu au kwa jina la Bwana Yesu (Mdo 2:38,10:48,19:5).
Nani anayestahili kubatizwa ?
- Mtu yeyote mwenye umri wa kuweza kuelewa na kumwamini Yesu na habari njema ya ufalme wa Mungu,kisha na kufahamu kikamilifu juu ya dhambi alizonazo ili aweze kutubu.
- Aliyeamini.
- Atubu kikamilifu ( Matendo 2;38)
Je watoto wachanga wanabatizwa?
Biblia imenyamaza kuhusu ubatizo wa vichanga kwa sababu ubatizo wa maji ni tendo la imani,na watoto wachanga hawana uwezo wa kuamini.Watoto wanabarikiwa na kuwekwa wakfu na mchungaji (Marko 10:13-14). Wale wanaobatiza kwa maji machache au watoto wanasimamia pale ambapo biblia imesema “akabatizwa na nyumba yake” kwa hiyo neno “nyumba yake” wanajumuisha pamoja na watoto wadogo mfano Matendo 16:33,lakini biblia hakutaja wazi humo ndani ya nyumba kulikuwa na watoto au lah! Hakuna mfano wa ubatizo wa vichanga au maji machache kwenye biblia hata mmoja,isipokuwa mfano uliwekwa na Yesu mwenyewe ni ubatizo wa maji mengi ukihusisha imani.
Matokeo ya ubatizo wa kikristo/wa maji mengi.
- Kutimiza sehemu ya agizo kuu la Bwana -(Mathayo 28;18-19)
- Kuzifia dhambi -( Warumi 6 :4)
- Picha ya wokovu (1 Petro 3:20-21)
- Kumvaa Kristo ( Wagalatia 3:27)
- Kuingizwa kwenye mwili wa Kristo yaani kanisa.(Wagalatia 3:26-28,1 Wakorintho 12:13)
- Zipo nyingi,Unipigie kwa maalezo zaidi.
Ni hasara gani apatayo mtu asiyebatizwa kwa maji mengi?
- Kuwa na uzito mkubwa kwenye safari yako ya wokovu wako.
- Kuwa mkristo wa mashaka – mashaka ! n.k
Je ni wakati gani mtu abatizwe? Lini?- Mtu atabatizwa mara tu baada ya kuokoka na kupata mafundisho sahihi. Biblia haisemi kukawilisha ubatizo bali ufanyike mara moja ( Matendo 10:47-48).
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS