Unajimu na Kutafsiri Nyota

0
5K

Je? Mungu anasema nini kuhusu wao wanao tafsiri nyota kuweza kujua jinsi maisha yao yatakavyokuwa? Imo katika Biblia, Isaya 47:13-15 "Umechoka kwa wingi wa mashauri yako basi nawasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. Tazama watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao ndivyo itakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale walio fanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wakukuokoa." 

Unajimu ni imani ambayo yafundisha kuwa uwambatano wa mwezi, nyota na jua waweza kuleta tukio katika maisha ya mtu. Katika lugha ya kiebrania neno unajimu ni kutabiri mbingu, kuweza kutoa siri, kutabiri jambo litakalotokea. Imo katika Biblia, Walawi 19:26 "...... Msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi." 

Kabla ya wana waisiraeli kuingia katika nchi ya ahadi, walionywa kutofanya unajimu, imo katika Biblia, Torati 18:9, 12, 14 "Utakapokwisha ingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale 12- kwamaana yule atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana Mungu wako anawafukuza mbele yako 14 maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanao shika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe Bwana, Mungu wako, hukupa ruhusa kutenda hayo." 

1Samueli 15:23 "Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyongo; kwa kuwa umelikataa neno la Bwana yeye naye amekukataa usiwe mfalme 

Wakati mfalme Nebukadreza alipo ota ndoto aliwaita wagana, wachawi, wasihiri na wakaldayo waweze kutafsiri ile ndoto. Imeandikwa Danieli 2:10 "Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme kwa maana hapana mfalme, wala bwana wala liwali aliyetaka neno hili kwa mganga wala kwa mchawi wala kwa mkaldayo." 

Imo katika Biblia, Danieli 2:27-28. "Danieli akajibu mbele ya mfalme akasema ili siri aliyoiuliza mfalme; wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu. Lakini yuko Mungu Mbinguni afunuaye siri naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayo kuwa siku za mwisho."

Search
Categories
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA
Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 07:12:46 0 5K
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 55 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:28:11 0 5K
DARASA LA 7
DARASA LA 7
Orodha ya masomo yote ya darasa la 7
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:17:36 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 22 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:16:50 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
What Is The Purpose Of Life?
Everybody has wondered at one time or another why they exist. What is my purpose in life? Is...
By GOSPEL PREACHER 2023-09-29 09:50:42 0 5K