Je ni nini kitawapata watu wale hawajawai pata nafasi ya kusikia kuhusu Yesu?

0
5Кб
Je ni nini kitawapata watu wale hawajawai pata nafasi ya kusikia kuhusu Yesu? Je Mungu atawahukumu wale ambao hajawai sikia kuhusu Yesu?"
 
Jibu: Watu wote wamewajibika kwa Mungu hata kama wamesikia au hawaja “sikia kumhusu” Bibilia yatwambia wazi wazi kuwa Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwa uungu (Warumi 1:20) na katika Roho za watu (Mhubiri 3:11). Shida ni kwamba ni uzao wa dhambi wa mwanadamu. Zote twakataa hii hekima ya Mungu na kuasi (Warumi 1:21-23). Kama isingekuwa ni neema ya Mungu, tungejitolea kwa mioyo ya dhambi, kujiruhusu kujigundulia vile maisha ni bure, yakustaajabisha ni sehemu kando naye Mungu. Anafanya haya kwa wale wanaoendelea kumkataa (Warumi 1:24-32).
 
Ukweli ni, si eti watu wengine hawajasikia juu ya Mungu. Badala, shida ni wamaekataa chenye wamesikia na chenye kinaonekana katika uumbaji. Kumbukumbu La Torati 4:29 yasema, “Lakini huko, kama mkimtatufa BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.” Aya hii yatufunza nguzo muimu. Kila mmoja anayemtafuta Mungu atampta. Kama mtu amenuia kumjua Mungu, Mungu atajudhihirisha kwake.
 
Shida pekee, “Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu” (Warumi 3:11). Watu wanakataa hekima ya Mungu ambayo ipo katika uumbaji na katika mioyo yao, na badala wanaanza kuabudu “miungu” yao wenyewe wamejitengenezea. Ni ubumpavu kubishana juu ya haki/uungwana wa Mungu kumtuma mtu jahanamu mwenye hakuwa na nafasi ya kuisikia injili ya Kristo. Watu watawajibika kwa Mungu kwa yale yote Mungu ameyafunua kwao. Bibilia inasema watu wanakataa hekima na kwa hivyo Mungu ako haki anapowahukkumu kwenda jahanamu.
 
Badala ya kujadiliana juu ya mwisho wa wale hawakusikia, sisi kama Wakristo yatupasa kufanya tuwezavyo wao kusikia injili wenye hawajaisikia. Tumeitwa kutangaza injili kwa mataifa yote (Mathayo 28:19-20; Matendo Ya Mitume 1:8). Tunajua kuwa watu wanakataa hekima ya Mungu ambayo imedhihirishwa kwao na hiyo inatusukuma kutangaza injili ya wokovu kupitia Yesu Kristo. Ni kwa kukubali neeme ya Mungu pekee kupitia Yesu Kristo watu wanaweza kuokolewa kutoka dhambini na kuepuka mauti ya milele pasipo na tumaini. Kama tutapuuza kuwa wale wote hawakusikia injili wameokolewa, haina tofauti wakati tunaakikisha kuwa hakuna mtu yeyote amepokea injili. Kitu kibaya zaidi tunaweza kufanya ni kushiriki injili na mtu na kumfanya huyu mtu aikatae hiyo injili. Kama hiyo ingekuwa itendeke, huyo mtu atahukumiwa. Watu wasioisikia injili watahukumiwa, la sivyo hatutakuwa na cha kututia moyo wa kuhiubiri injili. Mbona tujiatarishe watu kuikataa injili na kujihukumu wao wenyewe na hapo mbeleeni walikuwa wameokolewa kwa sababu hawakuwa wameisikia injili?
Поиск
Категории
Больше
SPIRITUAL EDUCATION
The Holy Spirit Dwells Within
I want to speak to you this month on the Holy Spirit. Today it will be "The Holy Spirit Dwells...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 18:34:26 0 5Кб
REVELATION
MAJIRA YA KANISA LA SARDI
(1) MLENGWA WA KANISAUFUNUO 3:1Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo...
От GOSPEL PREACHER 2021-09-24 10:07:38 0 6Кб
SPIRITUAL EDUCATION
Did Jesus speak in tongues?
No doubt, that is a question that has been asked by millions of Christians throughout...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:14:23 0 6Кб
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:35:09 0 6Кб
Networking
How to find great online marketplace ideas
Perhaps you already have a business idea that you can't get out of your mind. Or maybe you're...
От Business Academy 2022-09-17 03:34:39 0 7Кб