Je, Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?

0
5K
Matendo ya Mitume 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”
 
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
 
Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
 
Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46;Yohana 3:36).
 
Msamaha-Je, ni upate vipi?
 
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa ajili ya msamaha wetu.
 
Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
 
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
 
Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?
 
Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”
Cerca
Categorie
Leggi tutto
MASWALI & MAJIBU
Mitume Wote Waliopita Walikuwa Ni Watu Weupe Hata Manabii Wote Waliopita Hadi Ma-Papa Ni Ngozi Nyeupe. Ni Kweli Ngozi Nyeusi Ililaaniwa ?
JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:37:18 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
What does it mean that Jesus is the 'first-born' over Creation?
In a letter to the church at Colossae, the Apostle Paul gave an intriguing description of Jesus....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:23:01 0 5K
OTHERS
MBINU ZINAZOTUMIKA NA WAISLAMU ILI KUHARIBU IMANI YA KIKRISTO KATIKA KARNE YA 20-21 (21st CENTURY ISLAMIC STRATERGIES TO ELIMINATE/CORRUPT CHRISTIANITY IN AFRICA)
Utangulizi: Leo hii, ukitembea sehemu mbalimbali hapa duniani utakutana na waislamu wengi sana....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:27:52 0 6K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 17:54:08 0 6K
SPIRITUAL EDUCATION
Nawezaje kujazwa na Roho Mtakatifu?
Kifungu cha maana katika kuelewa juu ya kujazwa na Roho Mtakatifu in Yohana 14:16, mahali ampapo...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 11:04:02 0 5K