MASWALI NA MAJIBU KUHUSU DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU

0
6K

Kumekuwepo na mijadala mingi kila mahali na pia kumewepo na maoni mengi ya watu na mawao tofauti tofauti wanayotoa watu kuelezea kuhusu hii DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.Kwa leo sitazama kutoa ufahamu wa ndani zaidi kuelezea moja kwa moja kuhusu dhambi hii ila nitatumia mfumo wa maswali na majibu kuweza kuelezea kuhusu dhambi hii.IKiwa utahitaji kupata maelezo ya kina na kichambuzi basi tembelea link hii (UFAHAMU KUHUSU DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU) Ili kujifunza somo lote linalohusiana na UFAHAMU WA DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU

Lakini nitatumia mfumo wa maswali kuelezea mitizamo mbalimbali ya watu wanayotamani kujua kuhusu hii dhambi ya Kumkufuru Roho mtakatifu.Kwasababu ya tafsiri mbalimbali wanazoziweka watu wasiojua kutafsiri maandiko na kuelewa maana iliyokusudiwa , wamejikuta wakiwatwisha waumini wao au kuita watumishi Fulani kuwa wamefanya dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu hata kufikia hatua ya kuwatenga na kuwahesabu sio watu hata wa kuwapa salamu kwasababu ya hicho wanachodai wamemkufuru Roho mtakatifu hivyo hawawezi kusamehewa

Na kutokana na tafsiri hizo potofu kumekuwepo na watu wengi wanaoshindwa kufikiria toba au kurudi kwenye toba ya kweli kwasababu wameelezwa kuwa wamemkufuru Roho mtakatifu kwa kufanya dhambi Fulani Fulani ndani ya kanisa, ikiwa ni Kuzini, kubaka, kutoa mimba, kuua, kunywa pombe n.k.Lakini ni makusudi ya somo hili kupitia maswali na majibu mbalimbali kuweza kuelewa biblia na kuachana na tafsiri potofu zinazozagaa kila kona kuwafungia watu mzigo mzito wasitubu na kumrudia Mungu wao kwa dhambi walizoifanya

1} JE MTUMISHI ANAYEFUNDISHA IMANI POTOFU NA KUWAPOTEZA WATU WENGI ANAMKUFURU ROHO MTAKATIFU?
Si kila mtumishi anayefundisha mafundisho potofu na kuwapoteza watu kutokana na Imani potofu au kuitafsiri biblia vibaya eti nae anamkufuru Roho mtakatifu.

Huyu mtumishi ikiwa akijakufunuliwa juu ya kweli na kutubu ana uwezo kabisa akasamehewa Wengine wanafanya wanayoyafanya kutokana wamevaliwa tu nguvu za giza na nguvu za shetani hivyo wanajikuta wanafanya vituko hata kumtukana Mungu na kuleta mafundisho potofu kwa faida yao wenyewe

Shetani kwa makusudi akidhamiria kutoka ndani akiwa na ufahamu wake wote wala hakuvamiwa na Nguvu yeyote isipokuwa tamaa zake ndio aliamua Kufanya dhambi hii ya Kumkufuru Roho mtakatifu

Vivvyo hivyo Lazima Mtumishi huyo anayemkufuru isiwe imetokana na uvamizi tu wa mapepo alioupata au ukosefu wake tu wa maarifa ya kweli ya Neno la MUNGU ila akiwa na ufahamu na akili yake na utashi wake hali akiijua kweli na vipawa vyote vya Roho mtakatifu anaamua kubadilika kwa kuanza kumuhubiri shetani badala ya Mungu aliyekuwa anamuhubiri mwanzo na kufanikiwa kushawishi sehemu kubwa ya watu walio nyuma yake katika kanisa la Mungu.

2} JE KILA MTUMISHI WA MUNGU ANAWEZA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU?
Pia sio kila mtumishi wa Mungu anaweza kufanya dhambi hii eti asisamehewe.Wengine wanaweza wakawa wanawapotosha tu watu kutokana kushindwa kulielewa neno hivyo kujikuta yupo kwenye imani potofu kutokana na upotofu aliofundishwa na waalimu wa uongo tangu anaanza kumfrahamu Mungu hivyo kujikuta anaendelea kukaa kwenye hilo hilo Neno la upotofu alilowahi kujifunza kutokana na wachungaji wake au waalimu wake waliomfundisha mwanzo hivyo kupelekea hata akikua na kuitwa katika utumishi bado anaendelea kufundisha upotofu

Si kila mtumishi wa MUNGU ambaye yupo kwenye IMANI POTOFU na anaamini imani hizo potofu eti anakuwa amemkufuru Roho mtakatifu

3} JE,NI MTUMISHI MWENYE SIFA ZIPI ANAYEWEZA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU?
Kwanza yeye mwenyewe anaifahamu kweli hata kufikishwa viwango vya juu na Roho mtakatifu na kutembea na Mungu kwa uwazi na hata Mungu kumwamini kwenye mambo mengi akiwa na ushawishi mkubwa kwa sehemu kubwa hata ya dunia au eneo kubwa kutokana na kazi za Mungu zinazozihirika ndani yake.

Sasa mtumishi huyo kwa makusudi akigeuka akijua kabisa kweli ni ipi na kuanza kuwaelekeza watu kwa shetani kutokana na ushawishi na kuaminika kwake aliko nako , huyo ndiye ana uwezekano wa kumkufuru Roho Mtakatifu.

4} JE MTUMISHI WA MUNGU AKIRUDI NYUMA NA KUCHA WOKOVU NI KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU KWAMBA HATASAMEWEWA KABISA KAMA INAVYOSEMA WAEBRANIA 10:26-29?

WAEBRANIA 10:26-29 “Maana, KAMA TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI BAADA YA KUUPOKEA UJUZI WA ILE KWELI, HAIBAKI TENADHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu,na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”

Kutenda dhambi ya kukusudia baada ya kuifahamu ujuzi wa ile kweli inayozungumzwa katika maandiko hayo kwamba yanasema haibaki tena dhabuhu kwa ajili ya dhambi, kimsingi hapo haizungumzii KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU kwamba KUTOKUSAMEHEWA KABISA bali inazungumzia Juu ya dhambi ya Kumkana Yesu kwa kuamua KURUDI NYUMA DHAMBINI NA KUACHA WOKOVU ndio inaitwa KUMFANYIA JEURI ROHO MTAKATIFU sio Kumkufuru Roho mtakatifu tulikokuelezea

Kimsingi kinachozungumzwa hapo ni dhambi ya Kurudi nyuma anayoweza kufanya mtumishi wa Mungu ambaye amekwishawai kupokea wokovu, hivyo anapoamua kufanya dhambi kwa kusudi na kuendelea kuishi mbali na wokovu, anaweza kukabiliana na adhabu kali na nzito tofauti na mtu ambaye hajawai kupokea wokovu kabisa.Anaweza kupata mapigo mbalimbali kutokana na dhambi yake hiyo

Lakini KURUDI NYUMA kwa mtumishi wa Mungu hakumuhesabiwi kuwa AMEMKUFURU ROHO MTAKATIFU , ndio maana maandiko yanataja kama Kumfanyia Jeuri tu Roho mtakatifu.Hivyo mtumishi wa namna hiyo anaweza kabisa kutubu na akasamehewa ingawa kwa toba nzito, kwa namna ile ile ya PETRO alivyomkana Yesu mara 3 tena kwa kusudi, Pale alihesabika amerudi nyuma kwa kumfanyia jeuri Roho mtakatifu lakini , tunaona alivyoenda kwenye toba nzito alisamehewa kabisa, na ndivyo ambavyo YUDA ISKARIEOTE naye ikiwa angeenda mbele za Mungu kwa Toba nito ya namna ile ya Petro angesamehewa kabisa {MATHAYO 26:75}

5} JE KILA MTUMISHI AKITENDA DHAMBI KWA KUKUSUDIA ANAFANYA DHAMBI YA ROHO MTAKATIFU NA HAIBAKI TENA DHABIHU YA DHAMBI KWA AJILI YAKE? WAEBRANIA 10:26-29

Kinachozungumzwa hapo kuwa Haibaki tena ya dhambi kwa ajili ya huyo mtu aliyetenda dhambi kwa kukusudia sio kutokusamehewa kabisa kwa namna ile ya Kumkufuru Roho mtakatifu bali inazungumzia ugumu wa kupata msamaha kwa haraka tofauti na dhambi nyingine tunazofanya bila kukusudia, ikiwa mtu ataenda kutubu baada ya kufanya dhambi hiyo kwa makusudi

Mtumishi yeyote akifanya dhambi kwa kusudi eti kuwa atatubu baadae baada ya kufanya dhambi hiyo, huwa msamaha kwa mtu atendaye hayo hauji kiwepesi, yaani inakuwa ngumu sana kwake kupata amani ya moyo ya kusamehewa dhambi hiyo aliyotenda kwa makusudi ikiwa atatubu tu kwa kawaida kama anavyotubu au kujitakasa kwa dhambi nyingine.Mtu ataendelea kuwa na hukumu ndani yake hata baada ya kutubu

Mfano Esau alipouza uzaliwa wake wa kwanza aliutafuta kwa machozi lakini hakuupata WAEBRANIA 12:16-17, hapo inazungumzia toba ya dhambi aliyofanya kwa makusudi jinsi isivyo rahisi kupata msamaha kwa haraka na kuwa na amani kwa haraka hivyo kirahisi rahisi ingawa haimaanishi ukiuza uzaliwa wako wa kwanza yaani ukiacha wokovu kwa kufanya uasherati kama Esau eti hautasameheka kabisa ikiwa utatubu kwa toba nzito

Ni kweli dhambi zinazotendwa kwa kukusudia ni dhambi ambazo ni vigumu sana kupata amani moyoni mwako kwa toba ya kawaida, itampasa mtu kufanya toba nzito na inaweza kumchukua muda mrefu mpaka kupata hakika moyoni mwake ya kusamehewa dhambi hiyo

Kwa mfano Daudi historia inaeleza alivyofanya Uzinzi na mke wa URIA, ilimchukua karibu miaka 7 mpaka kuja kupata msamaha kwa ajili ya uovu alioufanya pamoja alikuwa anatubu na kulia sana mbele za Mungu.

Si maanishi nyakati hizi nasi itachukua muda huo kama wa daudi ila bado dhambi ukitenda kwa kukusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli ni vigumu sana kupata msamaha na amani ya moyo kwa kutubu kwa kawaida kama unavyotubia dhambi nyingine.

Turudi kwenye maandiko yanasemaje sio mitizamo yetu

MATHAYO 12:31-32 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”

Hapa Yesu anazungumza mambo mawili

1}Kumkufuru Yesu ambapo utasamehewa

2}Kumkufuru Roho mtakatifu ambapo hutasamhewa hata milele

Kumbuka huwezi kusamehewa ikiwa hujaomba msamaha wa kusamehewa yaani hujatubu. kwa msingi Huo hata huyo Anayemkufuru Yesu haiwezi kusema atasamehewa ikiwa hajatubu! Hivyo ukielewa kumbe hata kumkufuru Yesu ili usamehewe lazima utubu

Ila kwa kumkufuru Roho mtakatifu anavyosema hutasamehewa maanake HATA UKITUBU HUTASAMEHEWA KABISA HATA MILELE.Ndio maana Shetani hata leo akisema anatubu hatasamehewa

6} JE KWELI INAWEZEKANA MTUMISHI WA MUNGU AKAMKUFURU ROHO MTAKATIFU NA AKATUBU HASISAMEHEWE?
Biblia inatufundisha upo uwezekano wa mtu kuomba toba au Rehema lakini Mungu asiwasamehe wala kuwarehemu wala asiwasikilize

YEREMIA 7:16 “Basi, wewe usiwaombee watu hawa, wala usiwapazie sauti yako, wala kuwaombea dua(TOBA), wala usinisihi kwa ajili yao; KWA MAANA SITAKUSIKILIZA”

YEREMIA 14:10-12 “Bwana awaambia watu hawa hivi, Hivyo ndivyo walivyopenda kutanga-tanga; hawakuizuia miguu yao; basi, Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, atawapatiliza dhambi zao.Naye Bwana akaniambia, USIWAOMBEE WATU HAWA WAPATE HERI. WAFUNGAPO, MIMI SITASIKIA KILIO CHAO; NA WATOAPO SADAKA ZA KUTEKETEZWA NA SADAKA YA UNGA, SITAZITAKABALI; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.”

YEREMIA 15:1 “Ndipo Bwana akaniambia, HATA WANGESIMAMA MBELE ZANGU MUSA NA SAMWELI, MOYO WANGU USINGEWAELEKEA WATU HAWA; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.”

Hapa Mungu anaonyesha upo uweazekano wa kutowasikiliza kabisa wala kuwapatia rehema hata pale tutakapotaka kuwaombea rehema kwa kufunga ila Bwana hawasikia maombi ya namna hiyo

Sasa kwa nyakati za leo, Mungu anapokea toba ya mtu yeyote ikiwa akitubu isipokuwa ya kumkufuru Roho mtakatifu hiyo hata angesimama Musa na samweli watumishi wakubwa ambao Mungu anawaheshimu asingewasikia maombi yao.

7} JE MTUMISHI WA MUNGU AKIMKUFURU ROHO MTAKATIFU HATAWEZA KUFANYWA UPYA TENA HATA AKITUBU? NA JE ANAWEZA KUWA NA MSUKUMO WA KUTUBU TENA NDANI YAKE NA HASISAMEHEWE KABISA? Vipi kuhusu WAEBRANIA 6:6?
Ebu tuisome kwanza hiyo mistari inasemaje?

WAEBRANIA 6:6 Kwa maana hao WALIOKWISHA KUPEWA NURU, NA KUKIONJA KIPAWA CHA MBINGUNI, NA KUFANYWA WASHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU,NA KULIONJA NENO ZURI LA MUNGU, na nguvu za zamani zijazo,WAKAANGUKA baada ya hayo, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKATUBU; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

Hayo maneno HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKATUBU inaelezea jinsi isivyowezekana kumfanya mtu ambaye amemkufuru Roho mtakatifu kuweza kutubu maana ndani yake dhamiri yake inakuwa imechomwa moto au imekufa kabisa wala hakuna msukumo huo wa toba ndani yake maana amefanya dhambi isiyosameheka

Kitendo cha mtu aliyekwisha kuujua ujuzi wa nguvu za MUNGU kwa vipawa vyote vya Roho mtakatifu hata kusikia sauti ya Mungu na kuaminiwa na Mungu katika mambo mengi, mtu huyo huwezi kumfanya upya tena akatubu maana hakuna utakachomwambia ambacho hakijui maana amefanya kwa kujikinai kabisa kuanza kumuhubiri shetani badala ya Mungu na kuwaongoza watu kwa shetani badala ya Mungu.

Mtu huyu hata samehewa hata milele hata ingetokea akatubu japokuwa ni ngumu,ikiwa kweli alilofanya ni Kumkufuru Roho mtakatifu basi hatasamehewa hata akitubu

8} JE KWA HIYO INA MAANA KUNA WATU WALIOPO HAI AMBAO WAMESHAHUKUMIWA KAMA SHETANI, YAANI HAWANA MSAMAHA KWA MUNGU HATA WAKIWEZA KUIFANYA TOBA KWA KUMAANISHA BAADA YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU? UNAWEZA KUNIPA MIFANO YA WATU HAO AU WATUMISHI HAO WA MUNGU?
Kwanza, ni muhimu kuelewa dhambi hii ya kumkufuru Roho mtakatifu ni vigumu sana kuona kwa watu wa kawaida au watumishi wa Mungu wa kawaida kuifanya dhambi hii, kwa sababu ni ngumu sana kufanyika maana inaweza hata kuchukua vizazi na vizazi wasipatikane watu wa namna hiyo ambao Mungu amewaamini kwa namna kama ya Musa ambaye yeye alisema na Mungu uso kwa uso tofauti na watumishi wengine kama kina Miriamu na Haruni.

Ni dhambi ambazo zinaweza kufanywa na watumishi wa ngazi kama wakina Paulo mtume ambao Mungu ameweka wingi wa mafunuo ndani yao na kuaminiwa kwa viwango hata kuweza kutumika kuandika karibu nusu ya agano la kale, kufanya kazi kupita mitume wote n.k.Paulo ambaye ana ujasiri wa kuwaambia watu wamfuate yeye kama Yeye anavyomfuata kristo

Sasa kwa msingi huo unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo ilivyo vigumu watumishi wa ngazi hizo kutokea na kufanya dhambi hizo.

Unaweza ukanitajia mtumishi yeyote mwenye viwango hivyo vya kina Paulo mtume kiasi ambacho kilimfanya kuaminiwa kwa sehemu kubwa duniani kwa kuwaleta watu wengi kwa Yesu ambaye kwa ukengeufu akabadilika na kuanza kuwaambia watu wamfuate shetani?Utaona ni ngumu sana kutokea.

Ndio maana hata kwenye biblia hakuna mifano ya wazi ya watu waliotajwa moja kwa moja kuwa hawa walimkufuru Roho mtakatifu hivyo hawakusamehewa.Hivyo hata sisi tusiwawekee watu hatia na hukumu kwa kuwahesabia dhambii hii huku ni watu wenye msukumo wa kutubu.

Namkumbuka Mtumishi mmoja wapo anaitwa JIMMY SWAGGART mtumishi huyu si kwamba alimkufuru Roho Mtakatifu ila alikuwa mtumishi wa ngazi za juu sana ila itokea alifanya Uzinzi na kahaba mmoja.

Mhubiri huyu yupo mpaka sasa ni miongoni mwa watumishi waliokuwa wanahubiri na kukemea dhambi na hata kutumiwa na Mungu kwa viwango vya juu sana na ndiye amewafundisha wahubiri wengi kama kina BENNY HINN na hadi ana chuo cha biblia kikubwa tu huko kwao.

Ila aliweza kupatwa na kashfa hiyo ya kutembea na kahaba mmoja hotelini, jambo ambalo lilijulikana ulimwenguni kote.Lakini Mtumishi huyu wa Mungu pamoja na adhabu alizopewa za kinidhamu lakini alitubu sana na kuomba toba nzito sana mbele ya dunia mbele ya kanisa huku akiwa analia sana kwa kumkosea Mungu na wanadamu.Na mpaka sasa yupo amesamehewa na anaendelea kuhubiri sana utakatifu kwa viwango vya juu sana.

Hivyo nilitaka kusema Ikiwa mtumishi mkubwa na mwenye kuheshimika sana kama JIMMY SWAGGART aliweza kufanya ZINAA KOSA kuu na alipotubu Mungu alimsamehe sembuse sisi ambao tunajulikana tu kwenye kamtaa chetu au kwenye mkoa wetu au nchi yetu na hatujafika viwango vya juu kama hawa huyu mtumishi niliyemuelezea?

Ndio maana hata sasa kama ilivyo ngumu kwenye biblia kukupa mifano ya watu kwa wazi wazi kuwa hawa ndio walimkufuru Roho Mtakatifu, ndivyo ilivyo hata sasa ni vigumu kuwapata watu au watumishi wa ngazi hizo ambao wamemkufuru Roho Mtakatifu moja kwa moja.

MIFANO WA WATUMISHI WA MUNGU WAKUBWA WALIORUDI NYUMA NA HATA WENGINE KUMTUKANA MUNGU ILA HAWAKUMKUFURU ROHO MTAKATIFU
Watumishi wa Mungu wengi ambao ndio tunaweza kuwaona kirahisi hata wengine wanafikia mahali kwa kutokufahamu ukweli kuhusu kumkufuru Roho mtakatifu ndio wanadanganyika kuwaita watumishi Fulani wamemkufuru Roho mtakatifu kwa sababu wamerudi nyuma na kuanza kutukana makufuru juu ya wokovu.Kurudi nyuma kwa mtumishi wa Mungu sio kumkufuru Roho Mtakatifu

Mtumishi wa Mungu anaweza kurudi nyuma na kufanya vituko na mambo ambayo hata mataifa hawezi kufanya, na anaweza kumtukana Mungu hata kuutukana Wokovu lakini akawa bado hajamkufuru Roho mtakatifu.

Mtumishi au watumishi wa namna hiyo ndio tutawaona wako wengi ambao baada ya kufanya hayo nafsi zao na dhamiri zao zitawahukumu baada ya kupatwa na mapigo kadha wa kadha ndio tutawaona wanarudi na kutubu na badae wanaendelea vyema na wokovu.

Mfano Yupo MWINJILISTI MMOJA MKUBWA aliyefanya kazi pamoja na Paulo mtume anaitwa DEMA ambaye yeye hapo baadae alikuja kurudi nyuma na akaupenda ulimwengu kabisa 2TIMOTHEO 4:10, FILEMONI 1:25. Lakini Paulo hakusema amemkufuru Mungu.

Pia vile vile walikuwepo WATENDAKAZI WAKUBWA walifanya kazi kubwa nyakati za kanisa la Mungu ambao wao waliisukumia mbali imani hii ya wokovu hata kufikia hatua wakawa wanamtukana Mungu ambao walikuwa ni HIMENAYO NA ISKANDA.

Lakini Vile vile Paulo hakusema wamemkufuru Mungu bali alimtolea watu hao shetani ili awafundishe wasimtukane Mungu ili baada ya kufundisha wageuke na kumgeukia Mungu 1TIMOTHEO 1:20

Hivyo nasi, kadiri inavyowezekana tutafute kuwarejeza tena hasa hao wanaorudi Nyuma kuwafanya upya kwa kutubu dhambi zao, sio kuwahukumu na kuhesabu kuwa wamemkufuru Mungu eti kwasababu amefanya uzinzi au dhambi fulani kubwa na ya aibu.Bali kwa upole tuwaombee, tuwakumbushe kupendo wao wa kwanza, matendo mema waliyokuwa wanayafanya kabla ya kurudi nyuma na kuwahimiza kuutafuta uso wa Mungu kwa Kutubu. MUNGU AKUBARIKI.

Love
1
Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:26:48 0 6K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 30
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-26 05:15:15 0 5K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-01 18:37:24 0 5K
OTHERS
ALLAH ANAAPA KWA ALIYE UMBA KIUME NA KIKE
JE, NANI KAUMBA KIUME NA KIKE?QURAN 92 1-3 Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:39:34 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:09:00 0 5K