UFAHAMU KUHUSU DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU

4
8K

VIPENGELE VYA SOMO

(1). NI MAANA YA KUKUFURU?

(2). DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU IKOJEE?

(3). DHAMBI YA KUMKUFURU MUNGU ILIFANYWA NA SHETANI NA MALAIKA ZAKE WALIOASI


UTANGULIZI
Kumkufuru Roho mtakatifu ni dhambi nyingine mbaya sana tena kubwa zaidi ambayo haina msamaha milele na milele.

Na ole kwake kwa mtu yule atakayeitenda itakuwa imekula kwake.

Maana hata ukiitubu dhambi hii, haina msamaha kabisa.

M A T H A Y O 12:31-32:- " Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao."

M A R K O 3:28-29 “Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele".

Kumkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi isiyosameheka.

(1). NINI MAANA YA KUKUFURU?
Kwanza ni muhimu tufahamu kwanza neno hili "KUKUFURU" maana yake ni nini? Neno "KUKUFURU" au kwa kiyunani "Blasphe`mia" maana yake ni kutukana, kuzungumza vibaya, kudharau, kudhihaki na kukashifu ile imani au hicho kitu ulichokijua hapo mwanzoni na kukiamini au kukikubali.

Sasa mtu anapogeuka na kuanza kuwa kinyume nayo kwa kuiponda na kuisemavyo ovyoo hiyo imani au hicho kitu. Kwa lugha nyingine tunasema mtu huyo ameikufuru hiyo imani.

Kwa maana hiyo hata Biblia inaposema kwa mfano "Kumkufuru Mungu" maana yake ni kumtukana Mungu au kumdharau na kuzungumza vibaya juu ya Mungu . Huko ni kukufuru ! Na adhabu ya ki-biblia kwa mtu aliyethibitika kumkufuru Mungu alikuwa hana msamaha, adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa. Duhu! Hatari! [Soma:- WALAWI 24:10-16].

KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU:- Ni kumuasi huyo Roho Mtakatifu kwa kugeuka na kuwa kinyume naye huku ukizikana , ukiziponda na kuziharibu kazi zake.

Ni muhimu kufahamu kwamba Roho Mtakatifu ndiye mtendaji mkuu na mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika mwili wa Kristo duniani . Yeye ndiye anayeiwaita watu mbalimbali kwa kuwafanya kuwa watumishi wake hata kwa kuwapa upako huu au ule au kuwatia mafuta kihuduma katika kazi ya Mungu waliyoitiwa . Roho yeye ndiye anayewainua na kuwatumia kwa viwango tofauti kwa kipimo cha neema kama kila mmoja alivyopokea kwake .

LUKA 4:18:- "Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa."

1 WAKORINTHO 12:4-11, 28-30:- "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye...."

MATENDO 13:2:- "Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia."

Dhambi ya kumkufuru Roho haiwezi kufanywa na watu ambao bado hawajaokoka.

Wala Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa na mkristo yoyote tu wa kawaida ambaye hajainuliwa na Mungu katika ngazi yoyote ya utumishi katika huduma iliyowekwa na Mungu ndani yake.

(2). DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU IKOJEE?
Dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu inawalenga hasa zaidi watumishi wa Mungu wakubwa ambao wameinuliwa sana na Mungu kihuduma kwa kupewa neema iliyo kubwa zaidi ya wengine katika kanisa. Watu wa namna hii ndiyo wanaweza kuanguka kwenye dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.

Sasa watumishi hawa wa Mungu walioinuwa zaidi kihuduma kwa kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu mwenyewe. Wanapoanguka kiroho na kubadilika kuwa watumishi wa shetani huku wakiwavuta na kuwapoteza watu wengi kiroho mbali na Mungu aliye hai waliyemuhubiri hapo mwanzoni . Sasa hapo wanakuwa wameanguka katika dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Biblia inasema juu ya hilo katika

WAEBRANIA 6:4-8:- "Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, WAKAANGUKA BAADA YA HAYO , haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri."

Neno hilo "WASHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU" ni watu wale wanaotenda kazi pamoja na Roho Mtakatifu, yaani watumishi wa Mungu waliyoitwa kwa kupewa karama ya huduma hii au ile kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo.

Kumbuka ya kwamba watu wa namna hii ni wale watumishi ambao walikuwa na ushirika mkubwa sana na MUNGU. Kiasi kwamba Kazi zote za Roho mtakatifu zilikuwa zimedhihirishwa ndani yao kihuduma, na wenye kukionya kipawa cha mbinguni, maana yake waliaminiwa sana na Mungu hata akawachukua na kuwaonyesha live mbingu ilivyo, maana yake walipata mafunuo mengi ya kimbingu kwa kutwaliwa (2WAKORINTO 12:1-4). Wenye kuwasiliana na Mungu kupitia Roho mtakatifu. Alafu wakaanguka haiwezekani wakafanywa upya tena hata wakatubu.

Sasa watumishi hawa wanapoanguka kiroho dhambini na kubadilika kuwa watumishi wa shetani. Utaanza kuona yule Yesu waliyemuhubiri hapo mwanzoni na lile neno la kweli la utakatifu walilowahubiri watu hapo mwanzoni, wakaliamini na kuokolewa; watapingana nalo , na sasa wataanza kunena au kufundisha mambo mengine ya upotovu yaliyo dhahiri kinyume kabisa na ile kweli waliyoihubiri huku wakishawishi na kuwavuta watu, wafuasi wao, waumini au washirika wao mbali na njia ya kweli ya wokovu waliyoihubiri hapo mwanzoni . Na kwa sababu hapo mwanzoni walikuwa ni watumishi wa Mungu wazuri waliotumiwa sana na nguvu za Mungu , wanapoanguka kiroho na kugeuka na kuwa watumishi wa shetani. Utaweza kuona ni rahisi zaidi watu wengi mno kupotezwa nao kirahisi kwa sababu waliaminika sana. Sasa huko ndiko kunakoitwa "Kumkanyaga mwana wa Mungu na kumfanyia jeuri Roho wa neema ". Haaha! Inatisha!

WAEBRANIA 10:26-29:- "Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?"

1TIMOTHEO 5:15:- " Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani."

ISAYA 63:10:- "Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao."

Ni muhimu kufahamu kwamba Shetani hapo mwanzo kabla hajaasi mbinguni. Yeye alikuwa ni malaika mkuu mbinguni aliyekuwa anaitwa kwa jina la "LUCIFER. Shetani hapo mwanzo hakuwa adui wa Mungu kama ilivyo leo . Yeye aliumbwa na Mungu kama walivyoumbwa malaika wengine. Kiumbe huyu huko mbinguni alifanywa kuwa malaika mkuu na akapewa utukufu mwingi sana na Mungu zaidi ya malaika wengine.

Anatajwa kuwa "Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto". Aliyemtia mafuta Lucifer au kumtawadha kuwa malaika mkuu alikuwa ni Roho Mtakatifu mwenyewe yeye ndiye aliyemuinua na kumpa utukufu huo, akatumika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu akiwaongoza majeshi yoote ya malaika wa Mungu kumsifu na kumwabudu Mungu.

Hatimaye kiumbe huyu kwa sababu ya uzuri wa utukufu wa ukuu wake aliokuwa nao kupita malaika wengine alikuwa na kiburi na tamaa ya ukubwa zaidi, akaona nafasi aliyoinuliwa haikumtosha, sasa akatamani kumpindua hata Mungu aliyemuumba.

Akata alingane na Mungu na awe hata mkubwa zaidi ya Mungu. Ili kufanikisha adhima yake hii mbovu akaanzisha uasi wa chini kwa chini kinyume na Mungu wake, akaanza kuwashawishi malaika wengine mbinguni wawe kinyume na Mungu.

Akafanikiwa kuwapata malaika wachache idadi yao kama theluthi moja (1/3) ambao walimuunga mkono Lucifer na kuwa kinyume na Mungu.

Malaika wengine wote waliobakia walikataa kujiunga na uasi wa shetani wakabakia kuwa upande wa Mungu wao. Sasa mbingu nzima ikawa imepasuka vipande viwili malaika waliokuwa upande wa Mungu na wale wengine waliojitenga na kuamua kuwa upande wa Lucifer .

Jambo hilo ilipofikia hapo. Mungu alimfukuza huyu kiumbe mbinguni pamoja na malaika zake kwamba waondoke lakini wao hawakutaka. Mungu akaamua kutumia nguvu ya kijeshi kumg'oa Lucifer na kumtupa nje ya mbingu haraka sana.

Akamwita Mikaeli-malaika mkuu wa vita na kumwagiza kwamba ahakikishe kwamba anaisafisha mbingu yote nzima kwa kuwaondoa malaika wote waasi waliokuwa upande wa Lucifer. Sasa Kiumbe huyu Lucifer alipoona hivyo akawashawishi malaika wachache waliokuwa upande wake kupigana na majeshi ya malaika wa Mungu na matokeo yake Lucifer na malaika zake walishindwa vibaya, wakapigika kweli kweli na kutupwa nje ya mbingu.

Hivyo akawa siyo malaika mkuu tena aliyekuwa na jina lake "Lucifer" ambalo maana yake ni anayetoa mwanga kama nyota ya alfajiri.

Mungu akamlaani kiumbe huyu na viumbe vyake wakawa ni mashetani au majini , wakabadilika na kuwa viumbe vyenye kutisha vyenye sura mbaya :- Nyoka, ng'e, vinyamkela n. k. Shetani alipotupwa hapa chini duniani, nia yake ya kumpindua Mungu katika utawala wake ilikuwa bado ipo pale pale .

Akawashawishi wanadamu nao tokea Edeni hata leo wamuasi Mungu na kwenda kinyume naye kwa kutomtii Mungu na kuyaishii mapenzi yake.

[EZEKIEL 28:13-19; OBADIA 1:3-4; UFUNUO 12:7-9; ISAYA 14:12-15; YOHANA 8:44].

Kwa maana hiyo dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu inawahusu watu ambao walikuwa ni watumishi wa Mungu wakubwa walioinuliwa na kutumiwa sana na Mungu wanapoanguka kiroho na kugeuka kuwa watumishi wa shetani huku wakizitenda kazi zake shetani na kuwavuta wengine kinyume na njia ya kweli ya Mungu aliye hai waliyoifuata hapo mwanzoni

Watu kama hao mpaka hapo wanakuwa wamefanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.

Na hata kama baadaye watakuja kutubu, hawana msamaha milele.

Maana kupitia kwao tayari wanakuwa wamishapoteza roho za watu wengi kwenda upotevuni-Jehanaamu. "Huku ndiko kunakoitwa kumwaga damu za watu wengi kiroho wasio na hatia". Na hivyo watumishi kama hao wana hukumu kubwa ya dhambi ya milele isiyosameheka

[2WAFALME 24:3-4; MATHAYO 18:5-6,10-14].


(3). DHAMBI YA KUMKUFURU MUNGU ILIFANYWA NA SHETANI NA MALAIKA ZAKE WALIOASI
Unajua shetani naye alipoasi hakusamehewa na Mungu mpaka leo kwa sababu anatajwa kuwa alifanya "DHAMBI ILIYO KUBWA ZAIDI". Biblia inasema juu ya hilo katika YOHANA 19:11:"Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye (shetani) aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi."

Dhambi iliyo kubwa zaidi inayotajwa hapo ambayo aliifanya shetani ilikuwa ni dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.Baada ya shetani na malaika zake kumuasi Mungu. Mungu aliwawekewa adhabu kali ya MOTO WA MILELE.

Ni muhimu kufahamu Mungu hakuumba moto wa milele kwa ajili ya mwanadamu, bali Mungu aliuweka moto wa milele kwa ajili tu ya shetani na malaika zake basi waliomuasi.

Na kama wanadamu leo tunahukumiwa kwenda motoni ni kwa sababu tu ya kufuata mkumbo usiotuhusu wa kuamua kumtii shetani na kumuasi Mungu wetu aliyetuumba.

Na hivyo adhabu iliyokuwa juu ya shetani inatupata na sisi pia ambao tumejiingiza kwenye mkumbo usiotuhusu.

Neno la Mungu linasema katika MATHAYO 25:41:- "Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.". [ UFUNUO 20:10-15 ].

Mungu Baba yetu alitupenda sana sisi wanadamu zaidi hata ya malaika. Ingawa shetani na malaika zake walipomuasi Mungu hawakupata nafasi yoyote ile ya kusamehewa, lakini mwanadamu amepewa nafasi kubwa zaidi ya kusamehewa kwa zake dhambi zote atakazozifanya, kama akimwamini Bwana Yesu, akatubu, atasamehewa na kuokolewa na damu ya Yesu itamtakasa kabisa dhambi zake zote [WARUMI 3:23-26; WAKOLOSAI 1:12-14; 1YOHANA 2:1-2].

Isipokuwa kwa dhambi hii moja tu ya kumkufuru Roho Mtakatifu iwapo kama mwanadamu akiitenda dhambi hii ambayo aliifanya pia shetani, hawezi hakasamehewa milele na milele.

Na kama tulivyokwisha kuona kwamba dhambi hii ya kumkufuru Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa na mkristo yoyote tu wa kawaida katika kanisa, bali ni dhambi hasa ambayo ni vyepesi kufanywa na watumishi wa Mungu wakubwa walioinuliwa sana na Mungu katika utendaji wa nguvu za Roho Mtakatifu katika huduma zao za kuwaongoza, kuwalisha na kuwasimamia kondoo wa Mungu.

Watumishi kama hao wanapokengeuka kiroho na kufanyika kuwa watumishi wa shetani huku wakiwavuta na kuwapoteza kondoo wengi wa Mungu kuacha ile njia ya kweli ya wokovu.

Hapo sasa mtumishi yoyote wa Mungu aliyefikia hatua hiyo , amefanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Ambayo haina msamaha milele.

AMANI YA KRISTO YESU IWE PAMOJA NA ROHO YAKO, AMINA.

Love
1
Buscar
Categorías
Read More
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:18:20 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
What will happen to those who die without hearing anything of Christ Jesus?
The Holy Bible makes it conspicuous and crystal clear that while there are might be people in the...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:15:50 0 5K
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 37 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:14:55 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 29
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 38 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:47:15 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Mitume Wote Waliopita Walikuwa Ni Watu Weupe Hata Manabii Wote Waliopita Hadi Ma-Papa Ni Ngozi Nyeupe. Ni Kweli Ngozi Nyeusi Ililaaniwa ?
JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:37:18 0 5K