Je! Kiongozi Wa Dini Anao uwezo Wa Kusamehe Dhambi?

0
6KB

SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti kumweleza dhambi zako?.kwasababu imeandikwa “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; (Yohana 20:23)”

JIBU: Kwa kuongezea hapo Bwana Yesu pia alisema..

Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”

Hapo tunaona Petro alipewa funguo za ufalme wa mbinguni za kufunga na kufungua,(ambazo ni sawasawa tu na kumwondolea na kumfungia mtu dhambi) na vivyo hivyo na mitume wengine wote waliosalia walipewa funguo hizo hizo, lakini haikuwa na maana kuwa “wanao uwezo wa kumwondolea mtu dhambi kwa kumtamkia tu basi” hapana! bali walipewa “FUNGUO” za kumfanya mtu kuondolewa dhambi zake(UELEWA),, na ndio maana Petro na mitume wengine walipowahubiria watu na kuamini moja kwa moja waliwaambia WATUBU na WAKABATIZWE KILA MMOJA WAO KWA JINA LA YESU KRISTO ili dhambi zao ziondolewe (Matendo 2:38) lakini hawakuwaambia..”Njooni sisi tumepewa uwezo wa kuwaondolea dhambi zenu hivyo pokeeni msamaha”….

Unaona hapo huo ufunguo ni UFUNUO/UELEWA wa jinsi ya kufanya dhambi za mtu ziondolewe, Na ndio huo wa kumuhubiria mtu atubu, kisha akishatubu akabatizwe, hapo ndipo dhambi zake zitakuwa zimeondolewa.

Lakini Papa na Mapadre, na baadhi ya viongozi wengine wa kidini hawafanyi kama mitume walivyofanya bali wao wanawatamkia tu watu kwamba wamesamehewa dhambi zao basi, bila kufuata mwongozo sahihi kwa kisingizio cha hayo maandiko ya kwamba wao wamepewa hayo mamlaka….(kutokana na kukosa UFUNUO wa Roho Mtakatifu ndani yao wanayatafsiri maandiko kwa akili zao ili kutimiza matakwa yao wenyewe.) Mungu atusaidie. Kwahiyo kiongozi yeyote wa kidini akikwambia umesamehewa dhambi zako, pasipo toba binafsi na ubatizo sahihi matamshi yake ni batili yakatae.

Ubarikiwe sana.

Rechercher
Catégories
Lire la suite
DANIEL
DANIELI 9
Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe; Katika sura hii tunaona...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-08 01:31:39 0 9KB
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 23 questions at the...
Par THE HOLY BIBLE 2022-03-19 20:31:26 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
The Holy Spirit Dwells Within
I want to speak to you this month on the Holy Spirit. Today it will be "The Holy Spirit Dwells...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 18:34:26 0 5KB
REVELATION
UFUNUO 17
Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia...
Par GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:05:54 0 6KB
Injili Ya Yesu Kristo
UBATIZO WA MAJI MENGI WA KIBIBLIA
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Par GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:42:55 0 6KB