Sabato Halisi Ni Lini, Je! Ni Jumapili Au Jumamosi?, Ni Siku Gani Itupasayo Kuabudu?

0
5χλμ.

JIBU: Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Wakristo hawahesabiwi haki mbele za Mungu katika siku, miezi au miaka ya kuabudia, aidha uabudu jumapili, jumatatu, jumamosi au jumatano huo ni utaratibu wa mtu tu! haimuongezei mtu chochote katika uhusiano wake na Mungu. Biblia inasema..  

Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”

 Na Pia inasema tena katika

Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”  

Hivyo Maana ya NENO sabato ni “Pumziko”, na pumziko kwa wakristo lipo rohoni, na mwokozi wetu Yesu yeye alituambia kuwa ndiye BWANA wa sabato (soma Mathayo 12:8), hivyo tukimpata YESU tumeipata SABATO au “pumziko letu la rohoni” na ndio maana anasema..  

Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Kwahiyo wanaoabudu jumamosi, au jumapili au jumatano hawafanyi makosa, ni utaratibu wao tu, mbele za Mungu wote wapo sawa, kwa mfano tunasoma katika biblia wakristo wakwanza waliiteua siku ya kwanza ya juma ( yaani JUMAPILI) kwa ajili ya kukusanyika na kufanya changizo pamoja na kumega mkate,ukisoma Matendo 20:7 na 1Wakoritho 16:1-2 utaona jambo hilo, hivyo kuteua siku fulani na kusema hiyo ndio Mungu anairidhia kuabudia zaidi ya siku nyingine, ni kutokuyaelewa maandiko.   kwasababu ibada halisi ipo rohoni na Mungu anaabudiwa katika roho na kweli, na sio katika siku maalumu au miezi maalumu au miaka maalumu bali ni kila saa na kila wakati mahali popote.  

Ubarikiwe sana.

Αναζήτηση
Κατηγορίες
Διαβάζω περισσότερα
HOLY BIBLE
What does it mean that Jesus is the Son of God?
Jesus is not God’s Son in the sense of a human father and a son. God did not get married...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:23:35 0 5χλμ.
Injili Ya Yesu Kristo
HAYA NDIYO MADHARA YA KUABUDU PICHA ZA WATU WALIOIGIZA SINEMA ZA YESU!
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, YESU anawapenda na pia MUNGU anawapenda na ROHO...
από GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:44:36 0 6χλμ.
PRE-UNIT
PRE-UNIT 1
List of all of subjects for pre-unit 1 students
από PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:08:46 0 6χλμ.
SPIRITUAL EDUCATION
KWARESMA IPO KIBIBLIA
KWARESMA IPO KIMAANDIKO?       Kwaresma ni nini?..Je! Kwaresma ipo katika...
από Martin Laizer 2025-03-11 02:12:09 2 3χλμ.
FORM 1
KISWAHILI : KIDATO CHA 1
Orodha ya mada zote za somo la Kiswahili kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha 1: BONYEZA HAPA...
από PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-31 17:17:30 0 7χλμ.