Bwana Aliposema Kuwa Yeye Ni “Mungu Wa Miungu” Alikuwa Na Maana Gani?..Je! Yeye Ni Mungu Wa Sanamu?

0
7K

JIBU: Tukisoma Kumbukumbu 10:17 inasema…

“Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa”.  

Hapa tunaona Mungu anajitambulisha yeye kama “Mungu wa miungu” sasa swali hawa miungu ni wakina nani?.   Bwana Yesu alisema mahali fulani katika kitabu cha Yohana,..  

Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?”  

Kwahiyo unaona hapo miungu inayozungumziwa hapo ni WATOTO WA MUNGU, (yaani sisi tuliomwamini yeye na kuoshwa kwa damu yake) inadhaniwa na wengi kuwa miungu iliyozungumziwa pale ni “SANAMU” LA! sivyo. Mungu hawezi akawa ni Mungu wa sanamu. Sanamu hata siku moja haziwezi zikampa Mungu utukufu, Na tunajua tabia za miungu ni lazima zifanane na Mungu, Hivyo basi kazi zile zile Mungu anazozifanya lazima na miungu izifanye, kwa mfano Mungu alitumia NENO lake kuumba na kufanya kila kitu na sisi vivyo hivyo kwa NENO lake tunaweza tukafanya kazi za Mungu vile vile kama yeye. Lakini tusipoweza kufanya hivyo inamaana sisi sio miungu kwasababu hatufanani na yeye. ni sawasawa tu na alivyojiita yeye ni MFALME wa wafalme, au BWANA wa mabwana.  

Kwahiyo ili sisi tuwe miungu lazima tuwe ni WATOTO WA MUNGU wenye tabia kama za kwake nazo ni: Upendo, Imani, Haki, Utakatifu, utu wema, kiasi n.k Wagalatia 5:22 hivyo tuzidi kutia bidii katika kumjua yeye ili tustahili kuitwa miungu.  

Maelezo haya unaweza kuyapata kwa njia ya video mwisho wa somo hili

Ubarikiwe sana.  

Zoeken
Categorieën
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
YESU ALIBADILI MWENENDO WA HISTORIA YOTE
Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 21:16:46 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA
Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 07:12:46 0 5K
UCHUMBA KIBIBLIA
KANUNI 10 ZA UCHUMBA WENYE KUFANIKIWA
KwanzaWewe na mwenzako mnaweza kuwa na sifa nyingi kama wachumba. Huenda mkijitazama na watu...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 10:32:02 0 6K
JOB
Verse by verse explanation of Job 34
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 23 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:14:29 0 6K
NDOA KIBIBLIA
MWANAMKE SIMAMA KWENYE NAFASI YAKO ILI UIPONYE NDOA YAKO
Namshukuru Mungu ambaye anazidi kunipa neema ya kuandika na kuandika masomo mbalimbali na pia...
By GOSPEL PREACHER 2021-12-16 12:14:48 0 6K